Ezekiel 37:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Ezekieli nilikumbwa na uzito wa nguvu ya Mwenyezi-Mungu, naye akaninyanyua kwa roho yake na kuniweka katika bonde lililokuwa limejaa mifupa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho wa Mwenyezi Mungu na kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Ezekieli nilikumbwa na uzito wa nguvu ya Mwenyezi-Mungu, naye akaninyanyua kwa roho yake na kuniweka katika bonde lililokuwa limejaa mifupa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho wa BWANA na kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkono wa bwana ulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho wa bwana na kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika Roho ya BWANA, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo lilikuwa limejaa mifupa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Ezekieli nilikumbwa na uzito wa nguvu ya Mwenyezi-Mungu, naye akaninyanyua kwa roho yake na kuniweka katika bonde lililokuwa limejaa mifupa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkono wa Bwana ukanishika, Bwana akanitoa kirohoroho, akanipeleka na kuniweka katikati ya hilo bonde, nalo lilikuwa limejaa mifupa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya BWANA, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe alinijaza uwezo wake mimi Ezekieli. Roho wake akanitwaa na kunipeleka katika bonde lililokuwa limejaa mifupa.