Ezekiel 37:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe utawajibu, Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nitakitwaa kijiti cha Yosefu (kilichomo mkononi mwa Efraimu) na makabila ya Israeli yanayounganika naye, nami nitakishikamanisha na kijiti cha Yuda ili vijiti hivyo viwili vifanywe kijiti kimoja mkononi mwangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitaichukua fimbo ya Yusufu iliyo mkononi mwa Efraimu, na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye, na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa mmoja katika mkono wangu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na kabila za Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja mkononi mwangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe utawajibu, Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nitakitwaa kijiti cha Yosefu (kilichomo mkononi mwa Efraimu) na makabila ya Israeli yanayounganika naye, nami nitakishikamanisha na kijiti cha Yuda ili vijiti hivyo viwili vifanywe kijiti kimoja mkononi mwangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nitaichukua fimbo ya Yosefu, iliyoko mikononi mwa Efraimu na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa wamoja katika mkono wangu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Nitaichukua fimbo ya Yusufu, iliyoko mikononi mwa Efraimu na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa wamoja katika mkono wangu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na makabila ya Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja mkononi mwangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe utawajibu, Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nitakitwaa kijiti cha Yosefu (kilichomo mkononi mwa Efraimu) na makabila ya Israeli yanayounganika naye, nami nitakishikamanisha na kijiti cha Yuda ili vijiti hivyo viwili vifanywe kijiti kimoja mkononi mwangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona mimi, nikikichukua kijiti cha Yosefu kilichomo mkononi mwa Efuraimu nayo makabila ya Waisiraeli walio wenziwe, niwatie pamoja na kijiti cha Yuda, niwafanye kuwa kijiti kimoja tu; ndipo, watakapokuwa kimoja mkononi mwangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na kabila za Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja mkononi mwangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe utawajibu: Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitakitwaa kijiti cha Yosefu (kinachokuwa katika mukono wa Efuraimu) na makabila ya Israeli yanayoungana naye, nami nitakishikamanisha na kijiti cha Yuda kusudi vijiti hivyo viwili vifanywe kijiti kimoja katika mukono wangu.