Ezekiel 37:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawatoa Waisraeli kutoka mataifa walikokwenda; nitawakusanya toka pande zote na kuwarudisha katika nchi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kisha waambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wameenda. Nitawakusanya popote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawatoa Waisraeli kutoka mataifa walikokwenda; nitawakusanya toka pande zote na kuwarudisha katika nchi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kisha waambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wamekwenda. Nitawakusanya po pote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kisha waambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wamekwenda. Nitawakusanya popote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawatoa Waisraeli kutoka mataifa walikokwenda; nitawakusanya toka pande zote na kuwarudisha katika nchi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha uwaambie: Hivi ndivyo Bwana Mungu anavyosema: Mtaniona, nikiwachukua wana wa Isiraeli kwenye wamizimu, walikopelekwa, niwakusanye na kuwatoa pande zote; kisha nitawapeleka katika nchi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ukawaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na kuwaleta katika nchi yao wenyewe;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
uwaambie kwamba Bwana wetu Yawe anasema hivi: Nitawatoa Waisraeli kutoka mataifa walikokwenda; nitawakusanya toka pande zote na kuwarudisha katika inchi yao.