Ezekiel 37:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawatajitia unajisi tena kwa sanamu za miungu yao na kwa mambo yao ya kuchukiza wala kwa makosa yao. Nitawaokoa wasiwe tena waasi. Nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao, au vinyago vyao vinavyochukiza, wala kwa makosa yao yoyote, kwa maana nitawaokoa kutoka dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawatajitia unajisi tena kwa sanamu za miungu yao na kwa mambo yao ya kuchukiza wala kwa makosa yao. Nitawaokoa wasiwe tena waasi. Nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao na vinyago vyao visivyo na maana wala kwa makosa yao yo yote, kwa maana nitawaokoa kutoka katika dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao na vinyago vyao visivyo na maana wala kwa makosa yao yoyote, kwa maana nitawaokoa kutoka dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawatajitia unajisi tena kwa sanamu za miungu yao na kwa mambo yao ya kuchukiza wala kwa makosa yao. Nitawaokoa wasiwe tena waasi. Nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala hawatajipatia uchafu tena kwa kuyatambikia yale magogo yao wala kwa kuyafanya machukizo yao na mapotovu yao yote; nami nitawaokoa na kuwatoa mahali pao pote palipowakosesha, niwatakase; ndipo, watakapokuwa ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hawatajichafua tena kwa kuabudu sanamu za miungu yao na kwa mambo yao ya kuchukiza wala kwa makosa yao. Nitawaokoa wasikuwe tena waasi. Nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.