Ezekiel 37:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Ewe mtu, kwa niaba yangu toa unabii kwa upepo, ukauambie kwamba Bwana Mwenyezi-Mungu anasema hivi: Ewe upepo njoo toka pande zote nne na kuipuliza miili hii iliyokufa ili ipate kuishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo aliponiambia, “Utabirie pumzi; tabiri, mwanadamu na uiambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Njoo kutoka pande nne za pepo, ee pumzi, nawe upulizie pumzi ndani ya hawa waliouawa, ili wapate kuishi.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Ewe mtu, kwa niaba yangu toa unabii kwa upepo, ukauambie kwamba Bwana Mwenyezi-Mungu anasema hivi: Ewe upepo njoo toka pande zote nne na kuipuliza miili hii iliyokufa ili ipate kuishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo aliponiambia, “Utabirie upepo, tabiri, mwanadamu na uuambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Njoo kutoka pande nne, Ee pumzi, nawe upulizie pumzi ndani ya hawa waliouawa, ili wapate kuishi.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo aliponiambia, “Utabirie upepo, tabiri, mwanadamu na uuambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Njoo kutoka pande nne, ee pumzi, nawe upulizie pumzi ndani ya hawa waliouawa, ili wapate kuishi.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapulizie hawa waliouawa, wapate kuishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, Mwenyezi-Mungu akaniambia: “Ewe mtu, kwa niaba yangu toa unabii kwa upepo, ukauambie kwamba Bwana Mwenyezi-Mungu anasema hivi: Ewe upepo njoo toka pande zote nne na kuipuliza miili hii iliyokufa ili ipate kuishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia: Ufumbulie upepo! Fumbua, mwana wa mtu, ukiuambia upepo: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Wewe upepo njoo na kutoka pande zote nne za upepo, uwapuzie hawa waliouawa, wapate kuwa wazima tena!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, Yawe akaniambia: Ewe mwanadamu, kwa ajili yangu toa unabii kwa upepo, uuambie kwamba Bwana wetu Yawe anasema hivi: Ewe upepo kuja toka pande zote ine na kuipulizia miili hii iliyokufa kusudi ipate kuishi.