Ezekiel 38:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakazi wa Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vitongoji vyake watakuuliza, ‘Je, umekuja kuteka nyara? Je, umekusanya jeshi lako ili kushambulia na kutwaa nyara na kuchukua fedha na dhahabu, mifugo na bidhaa, na kuondoka na nyara nyingi?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sheba na Dedani, pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ili kuchukua nyara, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyang’anya mifugo na mali, na kuteka nyara nyingi zaidi?” ’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wana-simba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng'ombe na mali, kuteka mateka mengi sana?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakazi wa Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vitongoji vyake watakuuliza, ‘Je, umekuja kuteka nyara? Je, umekusanya jeshi lako ili kushambulia na kutwaa nyara na kuchukua fedha na dhahabu, mifugo na bidhaa, na kuondoka na nyara nyingi?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ya wajeuri ili kuchukua nyara mali, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyang'anya mifugo na mali na kuteka nyara nyingi zaidi?” ’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ya wajeuri ili kuchukua nyara mali, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyang’anya mifugo na mali na kuteka nyara nyingi zaidi?” ’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wanasimba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng'ombe na mali, kuteka kiasi kikubwa cha nyara?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakazi wa Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vitongoji vyake watakuuliza, ‘Je, umekuja kuteka nyara? Je, umekusanya jeshi lako ili kushambulia na kutwaa nyara na kuchukua fedha na dhahabu, mifugo na bidhaa, na kuondoka na nyara nyingi?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wasaba na Wadedani na wachuuzi wa Tarsisi na masimba yao wenye nguvu watakuuliza: Je? Umekuja kuteka mateka na kunyang'anya mali za watu? Umeikusanya mikutano yako kuchukua fedha na dhahabu, kujipatia ng'ombe na mali nyingine za watu, kuteka mateka mengi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sheba, na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi, pamoja na wana-simba wake wote, watakuambia, Je! Umekuja kuteka mateka? Umekusanya jeshi lako, ili kuwinda mawindo? Kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua ng’ombe na mali, kuteka mateka mengi sana?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wa Seba na Dedani pamoja na wachuuzi wa Tarsisi na wa vijiji vyake watakuuliza: Umekuja kunyanganya? Umekusanya kundi lako la waaskari kwa kushambulia na kutwaa mateka na kubeba feza na zahabu, makundi ya nyama na vitu, na kuondoka na vitu vingi?