Ezekiel 38:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utawakabili Waisraeli, kama wingu linalotanda juu ya nchi. Wakati huo nitakutuma uishambulie nchi yangu, ili mataifa yajue kwamba nimekutumia wewe Gogu ili nioneshe utakatifu wangu mbele yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionesha mtakatifu kupitia kwako mbele ya macho yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nawe utapanda juu uwajilie watu wangu, Israeli, kama wingu kuifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utawakabili Waisraeli, kama wingu linalotanda juu ya nchi. Wakati huo nitakutuma uishambulie nchi yangu, ili mataifa yajue kwamba nimekutumia wewe Gogu ili nioneshe utakatifu wangu mbele yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, Ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili kwamba mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionyesha mtakatifu kwa kukupitia wewe mbele ya macho yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili kwamba mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionyesha mtakatifu kwa kukupitia wewe mbele ya macho yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nawe utapanda juu uwajie watu wangu, Israeli, kama wingu likiifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kupitia kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utawakabili Waisraeli, kama wingu linalotanda juu ya nchi. Wakati huo nitakutuma uishambulie nchi yangu, ili mataifa yajue kwamba nimekutumia wewe Gogu ili nioneshe utakatifu wangu mbele yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utapanda kuwajia walio ukoo wangu wa Isiraeli, utaifunika nchi hiyo kama wingu. Siku zilizowekwa zitakapokwisha, nitakupeleka katika nchi yangu, kusudi wamizimu wapate kunijua mimi, nitakapojitokeza kuwa mtakatifu, nikikupatiliza, wewe Gogi, machoni pao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nawe utapanda juu uwajilie watu wangu, Israeli, kama wingu kuifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utawashambulia Waisraeli, kama vile wingu linalotanda juu ya inchi. Wakati huo nitakutuma uishambulie inchi yangu, kusudi mataifa yajue kwamba nimekutumia wewe Gogi kusudi nionyeshe utakatifu wangu mbele yao.