Ezekiel 38:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samaki baharini na ndege warukao, wanyama wa porini, viumbe vyote vitambaavyo pamoja na watu wote duniani, watatetemeka kwa kuniona. Milima itaporomoshwa, magenge yataanguka na kuta zote zitaanguka chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kinachotambaa ardhini, na watu wote walio duniani kote watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samaki baharini na ndege warukao, wanyama wa porini, viumbe vyote vitambaavyo pamoja na watu wote duniani, watatetemeka kwa kuniona. Milima itaporomoshwa, magenge yataanguka na kuta zote zitaanguka chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kitambaacho ardhini, na watu wote walio juu ya uso wa nchi watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kitambaacho ardhini, na watu wote walio juu ya uso wa nchi watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samaki baharini na ndege warukao, wanyama wa porini, viumbe vyote vitambaavyo pamoja na watu wote duniani, watatetemeka kwa kuniona. Milima itaporomoshwa, magenge yataanguka na kuta zote zitaanguka chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuniona watatetemeka samaki wa baharini na ndege wa angani na nyama wa porini na vidudu vyote vitambaavyo katika nchi nao watu wote wanaokaa katika nchi; ndipo, milima itakapoporomoka, nayo magenge yataanguka, nayo maboma yote yataanguka chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samaki na ndege, nyama wa pori, viumbe vyote vinavyotambaa pamoja na watu wote katika dunia, watatetemeka kwa kuniona. Milima itaporomoshwa, mawe yataanguka na kuta zote zitaanguka chini.