Ezekiel 38:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nitakuzungusha na kukutia ndoana matayani mwako, na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote: Farasi na wapandafarasi na kundi kubwa la watu wamevaa mavazi ya vita, ngao na vigao mikononi, wanapunga mapanga yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nami nitakugeuza na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nitakuzungusha na kukutia ndoana matayani mwako, na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote: farasi na wapandafarasi na kundi kubwa la watu wamevaa mavazi ya vita, ngao na vigao mikononi, wanapunga mapanga yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nami nitakugeuza na kutia ndoana katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nitakuzungusha na kukutia ndoana matayani mwako, na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote: Farasi na wapandafarasi na kundi kubwa la watu wamevaa mavazi ya vita, ngao na vigao mikononi, wanapunga mapanga yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitakugeuza nikikutia hatamu katika taya zako, nikutoe katika nchi yako pamoja na vikosi vyako vyote, farasi nao wawapandao, wao wote watakuwa wamevaa nguo za urembo, nao watakuwa mkutano mkubwa wenye ngao kubwa na ndogo, nao wote watashika panga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nami nitakugeuza na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi nitakugeuza na kukutia ndoana katika mataya yako, na kukutoa inje wewe pamoja na kundi lako lote la waaskari: farasi na waaskari wapanda-farasi na kundi kubwa la watu wanaovaa nguo za vita, ngao kubwa na ndogo katika mikono pamoja na mapanga yao.