Ezekiel 39:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Katika siku ile, nitampa Gogu mahali pa kuzikwa katika nchi ya Israeli, katika Bonde la Wasafiri, upande wa mashariki wa bahari ya Chumvi. Gogu atazikwa huko pamoja na jeshi lake lote, nao wasafiri watazuiwa kupita huko. Bonde hilo litaitwa, ‘Bonde la Hamon-gogu’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Siku ile nitampa Gogu mahali pa kuzikia katika Israeli, katika bonde la wale wasafirio upande wa mashariki mwa Bahari. Jambo hili litazuia njia ya wasafiri kwa sababu Gogu na makundi yake yote watazikwa huko. Kwa hiyo litaitwa Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na watu wake jamii yote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Katika siku ile, nitampa Gogu mahali pa kuzikwa katika nchi ya Israeli, katika Bonde la Wasafiri, upande wa mashariki wa bahari ya Chumvi. Gogu atazikwa huko pamoja na jeshi lake lote, nao wasafiri watazuiwa kupita huko. Bonde hilo litaitwa, ‘Bonde la Hamon-gogu’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Siku ile nitampa Gogu mahali pa kuzikia katika Israeli, katika bonde la wale wasafirio upande wa mashariki kuelekea baharini. Jambo hili litazuia njia ya wasafiri kwa sababu Gogu na makundi yake yote ya wajeuri watazikwa huko. Kwa hiyo litaitwa Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Siku ile nitampa Gogu mahali pa kuzikia katika Israeli, katika bonde la wale wasafirio upande wa mashariki kuelekea baharini. Jambo hili litazuia njia ya wasafiri kwa sababu Gogu na makundi yake yote ya wajeuri watazikwa huko. Kwa hiyo litaitwa Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na jamii ya watu wake wote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Katika siku ile, nitampa Gogu mahali pa kuzikwa katika nchi ya Israeli, katika Bonde la Wasafiri, upande wa mashariki wa bahari ya Chumvi. Gogu atazikwa huko pamoja na jeshi lake lote, nao wasafiri watazuiwa kupita huko. Bonde hilo litaitwa, ‘Bonde la Hamon-gogu’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo nitampa Gogi mahali pa kaburi kwao Waisiraeli katika bonde la wapitaji lililoko upande wa maawioni kwa jua kwenye bahari, nayo makaburi hayo yatawakinga wapitaji; ndiko, watakakomzika Gogi nao watu wake waliokuwa wengi, kisha watapaita Bonde la Wingi wa Gogi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, itakuwa katika siku hiyo, nitampa Gogu pa kuzikia katika Israeli, bonde la wapitao, upande wa mashariki wa bahari; nalo litawazuia wapitao; na huko watamzika Gogu na watu wake jamii yote; nao wataliita, Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ile, nitamupa Gogi pahali pa kufanyia maziko katika inchi ya Israeli, katika Bonde la Wasafiri, upande wa mashariki wa bahari ya Chumvi. Gogi atazikwa huko pamoja na kundi lake lote la waaskari, nao wasafiri watazuizwa kupita kule. Bonde hilo litaitwa, Bonde la Hamoni-Gogi.