Ezekiel 39:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya miezi hiyo saba, watachagua watu wapitepite nchini kutafuta maiti ambazo zitakuwa bado hazijazikwa, wazizike ili kuisafisha nchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Watu wataajiriwa mara kwa mara kuisafisha nchi. Baadhi yao watapita nchini kote, na, wakiwa na wengine, watawazika wale waliosalia juu ya ardhi. Mwisho wa hiyo miezi saba wataanza upekuzi wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya miezi hiyo saba, watachagua watu wapitepite nchini kutafuta maiti ambazo zitakuwa bado hazijazikwa, wazizike ili kuisafisha nchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Watu wataajiriwa mara kwa mara kuisafisha nchi. Baadhi yao watapita nchini kote na zaidi yao hao wengine, watawazika wale waliosalia juu ya uso wa nchi. Mwisho wa hiyo miezi saba wataanza upekuzi wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Watu wataajiriwa mara kwa mara kuisafisha nchi. Baadhi yao watapita nchini kote na zaidi yao hao wengine, watawazika wale waliosalia juu ya uso wa nchi. Mwisho wa hiyo miezi saba wataanza upekuzi wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watachunguza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya miezi hiyo saba, watachagua watu wapitepite nchini kutafuta maiti ambazo zitakuwa bado hazijazikwa, wazizike ili kuisafisha nchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha watachagua watu wa kushika kazi hiyo siku zote, watembee katika nchi, wawazike wapitaji wale waliosazwa juu ya nchi, wauondoe uchafu huo. Ile miezi saba itakapopita, ndipo, watakapochunguza,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watawachagua watu wa kufanya kazi ya daima, watakaopita kati ya nchi, ili kuwazika waliosalia juu ya uso wa nchi, ili kuisafisha; miezi saba itakapokwisha kupita watatafuta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha miezi hiyo saba, watatenga watu watakaopitapita katika inchi kwa kutafuta maiti ambazo zitakuwa bado hazijazikwa, wazizike kwa kuisafisha inchi.