Ezekiel 39:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wanapopitapita humo nchini, kama wakiona mfupa wa binadamu wataweka alama ili wale wanaozika waje na kuuzika katika Bonde la Hamon-gogu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanapopita nchini kote, na mmoja wao akaona mfupa wa mwanadamu, ataweka alama kando yake hadi wachimba kaburi wauzike katika Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao wapitao kati ya nchi watatafuta; na mtu ye yote aonapo mfupa wa mtu, ndipo atakapoweka alama karibu nao, hata wazishi watakapouzika katika bonde la Hamon-Gogu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wanapopitapita humo nchini, kama wakiona mfupa wa binadamu wataweka alama ili wale wanaozika waje na kuuzika katika Bonde la Hamon-gogu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wanapopita nchini kote na mmoja wao akaona mfupa wa mwanadamu, ataweka alama kando yake mpaka wachimba kaburi wawe wameuzika katika Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wanapopita nchini kote na mmoja wao akaona mfupa wa mwanadamu, ataweka alama kando yake mpaka wachimba kaburi wawe wameuzika katika Bonde la Hamon-Gogu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao wapitao kati ya nchi watachunguza; na mtu yeyote aonapo mfupa wa mtu, ndipo atakapoweka alama karibu nao, hadi wazikaji watakapouzika katika bonde la Hamon-Gogu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wanapopitapita humo nchini, kama wakiona mfupa wa binadamu wataweka alama ili wale wanaozika waje na kuuzika katika Bonde la Hamon-gogu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
watembezi wakitembea katika hiyo nchi; napo hapo, watakapoona mifupa ya mtu, watapajenga kando yake kichuguu, mpaka wazishi wamzike katika Bonde la Wingi wa Gogi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao wapitao kati ya nchi watatafuta; na mtu ye yote aonapo mfupa wa mtu, ndipo atakapoweka alama karibu nao, hata wazishi watakapouzika katika bonde la Hamon-Gogu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanapoona mufupa wa mutu wataweka kitambulisho juu yake kusudi wale wanaozika wakuje na kuuzika katika Bonde la Hamoni-Gogi.