Ezekiel 39:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Sasa nitawahurumia Waisraeli wazawa wa Yakobo, na kuwarudishia fanaka yao. Daima nataka jina langu takatifu liheshimiwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Sasa nitamrudisha Yakobo kutoka utumwani, nami nitawahurumia watu wote wa Israeli, nami nitakuwa na wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Sasa nitawarejeza watu wa Yakobo waliohamishwa, nitawahurumia nyumba yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina langu takatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Sasa nitawahurumia Waisraeli wazawa wa Yakobo, na kuwarudishia fanaka yao. Daima nataka jina langu takatifu liheshimiwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Sasa nitamrudisha Yakobo kutoka utumwani, nami nitawahurumia watu wote wa Israeli, nami nitakuwa na wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa hiyo hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Sasa nitamrudisha Yakobo kutoka utumwani, nami nitawahurumia watu wote wa Israeli, nami nitakuwa na wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Sasa nitawarejesha watu wa Yakobo waliohamishwa, nitawahurumia nyumba yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina langu takatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Sasa nitawahurumia Waisraeli wazawa wa Yakobo, na kuwarudishia fanaka yao. Daima nataka jina langu takatifu liheshimiwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Sasa nitayafungua mafungo yake Yakobo, niwahurumie wote walio mlango wa Isiraeli kwa kutenda wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Sasa nitawarejeza watu wa Yakobo waliohamishwa, nitawahurumia nyumba yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina langu takatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Bwana wetu Yawe anasema hivi: Sasa nitawahurumia Waisraeli wazao wa Yakobo, na kuwarudishia fanaka yao. Ninataka jina langu takatifu liheshimiwe siku zote.