Ezekiel 39:28 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, kwa sababu mimi niliwapeleka uhamishoni kati ya mataifa na kuwarudisha tena katika nchi yao. Sitamwacha hata mtu wao abaki miongoni mwa mataifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao, ingawa niliwapeleka uhamishoni miongoni mwa mataifa, nitawakusanya tena katika nchi yao wenyewe, bila kumwacha yeyote nyuma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao, kwa kuwa naliwahamisha, waende utumwani kati ya mataifa, na mimi nikawakusanya, na kuwaingiza katika nchi yao wenyewe; wala sitawaacha tena huko kamwe, hata mmojawapo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, kwa sababu mimi niliwapeleka uhamishoni kati ya mataifa na kuwarudisha tena katika nchi yao. Sitamwacha hata mtu wao abaki miongoni mwa mataifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi BWANA, Mungu wao, ingawa niliwapeleka uhamishoni miongoni mwa mataifa, nitawakusanya tena katika nchi yao wenyewe, bila kumwacha ye yote nyuma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi bwana, Mungu wao, ingawa niliwapeleka uhamishoni miongoni mwa mataifa, nitawakusanya tena katika nchi yao wenyewe, bila kumwacha yeyote nyuma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, kwa kuwa niliwahamisha, waende utumwani kati ya mataifa, na mimi nikawakusanya, na kuwaingiza katika nchi yao wenyewe; wala sitawaacha tena huko kamwe, hata mmojawapo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha watatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, kwa sababu mimi niliwapeleka uhamishoni kati ya mataifa na kuwarudisha tena katika nchi yao. Sitamwacha hata mtu wao abaki miongoni mwa mataifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nao watajua, ya kuwa mimi Bwana Mungu wao kweli naliwahamisha kwenda kwa wamizimu, lakini nitawakusanya tena, warudi katika nchi yao, sitasaza hata mmoja wao huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, kwa kuwa naliwahamisha, waende utumwani kati ya mataifa, na mimi nikawakusanya, na kuwaingiza katika nchi yao wenyewe; wala sitawaacha tena huko kamwe, hata mmojawapo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha watatambua kwamba mimi ni Yawe, Mungu wao, kwa sababu mimi niliwapeleka katika uhamisho kati ya mataifa na kuwarudisha tena katika inchi yao. Sitamwacha hata mutu wao mumoja abakie kati ya mataifa.