Ezekiel 39:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utakufa juu ya milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na mataifa yaliyo pamoja nawe. Nami nitaitoa miili yao iliwe na ndege wa kila aina na wanyama wakali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utaanguka kwenye milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na yale mataifa yaliyo pamoja nawe. Nitakutoa uwe chakula cha ndege wa aina zote walao nyama na cha wanyama pori.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa nchi, uliwe na wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utakufa juu ya milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na mataifa yaliyo pamoja nawe. Nami nitaitoa miili yao iliwe na ndege wa kila aina na wanyama wakali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utaanguka kwenye milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na yale mataifa yaliyo pamoja nawe. Nitakutoa uwe chakula cha ndege wa aina zote walao nyama na cha wanyama wa mwituni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utaanguka kwenye milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na yale mataifa yaliyo pamoja nawe. Nitakutoa uwe chakula cha ndege wa aina zote walao nyama na cha wanyama wa mwituni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa pori, uliwe na wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utakufa juu ya milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na mataifa yaliyo pamoja nawe. Nami nitaitoa miili yao iliwe na ndege wa kila aina na wanyama wakali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Milimani kwa Waisiraeli utaanguka wewe na vikosi vyako vyote nayo makabila, uliyo nayo; nitakutoa, uliwe nao ngusu na wote wenye mabawa na nyama wa porini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utaanguka juu ya milima ya Israeli, wewe, na vikosi vyako vyote, na watu wa kabila nyingi walio pamoja nawe; nami nitakutoa na kuwapa ndege wa kila namna walao nyama, na wanyama wa nchi, uliwe na wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utakufa juu ya milima ya Israeli, wewe pamoja na makundi yako yote ya waaskari na mataifa yanayokuwa pamoja nawe. Nami nitaitoa miili yao ikuliwe na ndege wa kila aina na nyama wakali.