Ezekiel 39:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitalifanya jina langu takatifu litambuliwe na watu wangu Israeli, wala sitaruhusu tena watu walikufuru jina langu takatifu. Nayo mataifa yatatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Nitalifanya Jina langu takatifu lijulikane miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitaliacha tena Jina langu takatifu litiwe unajisi, nayo mataifa watajua kuwa Mimi Mwenyezi Mungu ndimi Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa limejulika kati ya watu wangu Israeli; wala sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, na Aliye Mtakatifu katika Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitalifanya jina langu takatifu litambuliwe na watu wangu Israeli, wala sitaruhusu tena watu walikufuru jina langu takatifu. Nayo mataifa yatatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Nitalifanya Jina langu takatifu lijulikane miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitaliacha tena Jina langu takatifu litiwe unajisi, nayo mataifa watajua kuwa Mimi BWANA ndimi niliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Nitalifanya Jina langu takatifu lijulikane miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitaliacha tena Jina langu takatifu litiwe unajisi, nayo mataifa watajua kuwa Mimi bwana ndimi Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa limejulikana kati ya watu wangu Israeli; wala sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, na Aliye Mtakatifu katika Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitalifanya jina langu takatifu litambuliwe na watu wangu Israeli, wala sitaruhusu tena watu walikufuru jina langu takatifu. Nayo mataifa yatatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Jina langu takatifu watalijulisha kwao walio ukoo wangu wa Isiraeli, nami sitanyamaza tena, Jina langu takatifu likipatiwa uchafu; ndipo, wamizimu watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana aliye Mtakatifu kwao Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa limejulika kati ya watu wangu Israeli; wala sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, na Aliye Mtakatifu katika Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitajulisha jina langu takatifu kwa watu wangu Waisraeli, wala sitaruhusu tena watu walikufuru jina langu takatifu. Nayo mataifa yatatambua kwamba mimi ni Yawe, Mutakatifu wa Israeli.