Ezekiel 39:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, watu waishio katika miji ya Israeli watatoka na kukusanya silaha zilizoachwa na kuzichoma moto. Watatumia hizo ngao, pinde, mishale, mikuki na marungu, kama kuni za kuwasha moto kwa muda wa miaka saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, watu waishio katika miji ya Israeli watatoka na kukusanya silaha zilizoachwa na kuzichoma moto. Watatumia hizo ngao, pinde, mishale, mikuki na marungu, kama kuni za kuwasha moto kwa muda wa miaka saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani, kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani, kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, watu waishio katika miji ya Israeli watatoka na kukusanya silaha zilizoachwa na kuzichoma moto. Watatumia hizo ngao, pinde, mishale, mikuki na marungu, kama kuni za kuwasha moto kwa muda wa miaka saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, wakaao katika miji ya Waisiraeli watakapotoka, wavitumie vile vyombo vya vita kuwa kuni za kuwasha moto, zile ngao ndogo na kubwa, nazo pindi na mishale, nazo rungu na mikuki, wataitumia kuwa kuni za moto miaka saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, watu wanaoishi katika miji ya Israeli watatoka na kukusanya silaha zilizoachwa na kuzichoma kwa moto. Watatumia hizo ngao, pinde, mishale, mikuki na magongo, kama kuni za kuwasha moto kwa muda wa miaka saba.