Ezekiel 4:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo nikamwambia, “Ee, Bwana Mwenyezi-Mungu, kamwe sijajitia najisi kwa kula kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, wala sijapata kuonja nyama ya mnyama najisi tangu ujana wangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo nikasema, “Sivyo Bwana Mungu Mwenyezi! Kamwe mimi sijajitia unajisi. Tangu ujana wangu hadi sasa sijala kamwe kitu chochote kilichokufa au kilichoraruliwa na wanyama pori. Hakuna nyama yoyote najisi iliyoingia kinywani mwangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, tazama, roho yangu haikutiwa unajisi; maana tangu ujana wangu hata sasa sijala nyamafu, wala iliyoraruliwa na hayawani; wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo nikamwambia, “Ee, Bwana Mwenyezi-Mungu, kamwe sijajitia najisi kwa kula kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, wala sijapata kuonja nyama ya mnyama najisi tangu ujana wangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo nikasema, “Sivyo BWANA Mwenyezi! Kamwe mimi sijajitia unajisi. Tangu ujana wangu hadi sasa sijala kamwe kitu cho chote kilichokufa au kilichoraruliwa na wanyama wa mwituni. Hakuna nyama ye yote najisi iliyoingia kinywani mwangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo nikasema, “Sivyo bwana Mwenyezi! Kamwe mimi sijajitia unajisi. Tangu ujana wangu hadi sasa sijala kamwe kitu chochote kilichokufa au kilichoraruliwa na wanyama wa mwituni. Hakuna nyama yeyote najisi iliyoingia kinywani mwangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, tazama, roho yangu haikutiwa unajisi; maana tangu ujana wangu hata sasa sijala nyamafu, wala iliyoraruliwa na wanyama; wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo nikamwambia, “Ee, Bwana Mwenyezi-Mungu, kamwe sijajitia najisi kwa kula kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, wala sijapata kuonja nyama ya mnyama najisi tangu ujana wangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikasema: E Bwana Mungu, tazama, roho yangu haijatiwa uchafu; tangu hapo, nilipokuwa mtoto, mpaka sasa sijala kibudu wala makombo ya nyama wa porini, wala yenye uvundo hayajaingia kinywani mwangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, tazama, roho yangu haikutiwa unajisi; maana tangu ujana wangu hata sasa sijala nyamafu, wala iliyoraruliwa na hayawani; wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu nikamwambia hivi: Ee, Bwana wangu Yawe, sijajichafua hata kidogo kwa kula nyamafu wala nyama aliyeuawa na nyama wa pori, wala sijapata kuonja nyama anayehesabiwa kuwa muchafu tangu ujana wangu.