Ezekiel 4:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Chukua ngano, shayiri, maharagwe, choroko, mtama na mawele, uvitie vyote katika chombo kimoja, ujitengenezee mkate. Mkate huo ndio utakaokuwa chakula chako wakati unapolala kwa upande mmoja, siku zote 390.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Chukua ngano na shayiri, maharagwe na dengu, mtama na mawele, uviweke na kuvihifadhi vyote kwenye gudulia la kuhifadhia, na uvitumie kujitengenezea mkate. Utaula mkate huo kwa hizo siku mia tatu na tisini (390) utakazokuwa umelala kwa upande mmoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Pia ujipatie ngano, na shayiri, na kunde, na dengu, na mtama, na kusemethi, ukavitie vyote katika chombo kimoja, ukajifanyie mkate kwa vitu hivyo; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala ubavuni mwako; yaani, siku mia tatu na tisini utaula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Chukua ngano, shayiri, maharagwe, choroko, mtama na mawele, uvitie vyote katika chombo kimoja, ujitengenezee mkate. Mkate huo ndio utakaokuwa chakula chako wakati unapolala kwa upande mmoja, siku zote 390.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Chukua ngano na shayiri, maharagwe na dengu, mtama na mawele, viweke na kuvihifadhi vyote kwenye gudulia la kuhifadhia na uvitumie kujitengenezea mkate. Utaula mkate huo kwa hizo siku 390 utakazokuwa umelala kwa upande mmoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Chukua ngano na shayiri, maharagwe na dengu, mtama na mawele, uviweke na kuvihifadhi vyote kwenye gudulia la kuhifadhia, na uvitumie kujitengenezea mkate. Utaula mkate huo kwa hizo siku 390 utakazokuwa umelala kwa upande mmoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Pia ujipatie ngano, na shayiri, na kunde, na dengu, na mtama, na mawele, ukavitie vyote katika chombo kimoja, ukajifanyie mkate kwa vitu hivyo; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala ubavuni mwako; yaani, siku mia tatu na tisini utaula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Chukua ngano, shayiri, maharagwe, choroko, mtama na mawele, uvitie vyote katika chombo kimoja, ujitengenezee mkate. Mkate huo ndio utakaokuwa chakula chako wakati unapolala kwa upande mmoja, siku zote 390.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena jipatie ngano na mawele na maharagwe na choroko na mtama mweupe na mwekundu, uzitie zote katika chombo kimoja! Ndizo ujitengenezee mikate, kama hesabu ilivyo ya siku, utakazoulalia ubavu wako; siku 390 utaila hio mikate.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Pia ujipatie ngano, na shayiri, na kunde, na dengu, na mtama, na kusemethi, ukavitie vyote katika chombo kimoja, ukajifanyie mkate kwa vitu hivyo; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala ubavuni mwako; yaani, siku mia tatu na tisini utaula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe utwae ngano, shayiri, mahalagi, manjegere, mutama na ulezi, uvitie vyote katika chombo kimoja, ujitengenezee mukate. Mukate huo ndio utakaokuwa chakula chako wakati unapolala kwa upande mumoja, siku zote mia tatu na makumi kenda.