Ezekiel 40:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwaka wa ishirini na tano tangu kuhamishwa kwetu, siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, siku hiyo niliusikia uzito wa nguvu ya Mwenyezi-Mungu. Ilikuwa mwaka wa kumi na nne tangu mji wa Yerusalemu ulipotekwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa ishirini na tano wa uhamisho wetu, mwanzoni mwa huo mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kuanguka kwa mji, siku hiyo hiyo mkono wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yangu, naye akanipeleka huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu, mwanzo wa mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kupigwa mji, siku iyo hiyo, mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, akanileta huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwaka wa ishirini na tano tangu kuhamishwa kwetu, siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, siku hiyo niliusikia uzito wa nguvu ya Mwenyezi-Mungu. Ilikuwa mwaka wa kumi na nne tangu mji wa Yerusalemu ulipotekwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa ishirini na tano wa uhamisho wetu, mwanzoni mwa huo mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kuanguka kwa mji, siku hiyo hiyo mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanipeleka huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa ishirini na tano wa uhamisho wetu, mwanzoni mwa huo mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kuanguka kwa mji, siku hiyo hiyo mkono wa bwana ulikuwa juu yangu, naye akanipeleka huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu, mwanzo wa mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kupigwa mji, siku hiyo hiyo, mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, akanileta huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwaka wa ishirini na tano tangu kuhamishwa kwetu, siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, siku hiyo niliusikia uzito wa nguvu ya Mwenyezi-Mungu. Ilikuwa mwaka wa kumi na nne tangu mji wa Yerusalemu ulipotekwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa katika mwaka wa 25 wa kuhamishwa kwetu, mwaka ulipoanza, siku ya kumi ya mwezi, nao ulikuwa mwaka wa 14 wa kutekwa kwa huo mji, siku ileile ndipo, mkono wa Bwana uliponishika, ukanipeleka huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu, mwanzo wa mwaka, siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya kupigwa mji, siku iyo hiyo, mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, akanileta huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa makumi mbili na tano tangu tulipopelekwa katika uhamisho, siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, siku hiyo Yawe alinijaza uwezo wake. Ilikuwa mwaka wa kumi na ine tangu pale Yerusalema ulipotekwa.