Ezekiel 40:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na matundu madogomadogo kwenye miimo ya nje ya vyumba vyote na hata kwenye kuta zilizotenganisha vyumba. Kulikuwa na michoro ya mitende kwenye miimo ya ndani iliyoelekea ukumbi wa kupitia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulikuwa na vidirisha kwenye hivyo vyumba vya walinzi, na nguzo za hivyo vyumba zilikuwa kwenye mzunguko wa hilo lango; vivyo hivyo kulikuwa na madirisha yaliyozunguka kuelekeana na ua. Juu ya kila nguzo kulikuwa na nakshi za mitende.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa vile vyumba palikuwa na madirisha yaliyofungwa, na kwa miimo yake ndani ya lango pande zote, na kwa matao yake vivyo hivyo; na madirisha yalikuwako, pande zote upande wa ndani, tena palikuwa na mitende juu ya kila mwimo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na matundu madogomadogo kwenye miimo ya nje ya vyumba vyote na hata kwenye kuta zilizotenganisha vyumba. Kulikuwa na michoro ya mitende kwenye miimo ya ndani iliyoelekea ukumbi wa kupitia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulikuwa na vidirisha kwenye hivyo vyumba vya walinzi na nguzo za hivyo vyumba zilikuwa kwenye mzunguko wa hilo lango, vivyo hivyo kulikuwa na madirisha yaliyozunguka kuelekeana na ua na juu ya kila nguzo kulikuwa na mapambo ya miti ya mitende.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulikuwa na vidirisha kwenye hivyo vyumba vya walinzi na nguzo za hivyo vyumba zilikuwa kwenye mzunguko wa hilo lango, vivyo hivyo kulikuwa na madirisha yaliyozunguka kuelekeana na ua na juu ya kila nguzo kulikuwa na mapambo ya miti ya mitende.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa vile katika vyumba palikuwa na madirisha yaliyofungwa, na kwa miimo yake ndani ya lango pande zote, na kwa matao yake vivyo hivyo; na madirisha yalikuwako, pande zote upande wa ndani, tena palikuwa na mitende juu ya kila mwimo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na matundu madogomadogo kwenye miimo ya nje ya vyumba vyote na hata kwenye kuta zilizotenganisha vyumba. Kulikuwa na michoro ya mitende kwenye miimo ya ndani iliyoelekea ukumbi wa kupitia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Madirisha yenye vyuma yalikuwa kwenye vyumba na kwenye miimo upande wa ndani wa hilo jengo la lango po pote; nao ukumbi ulikuwa na madirisha po pote yaliyoelekea ndani. Penye nguzo palikuwa pamechorwa mitende.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa vile vyumba palikuwa na madirisha yaliyofungwa, na kwa miimo yake ndani ya lango pande zote, na kwa matao yake vivyo hivyo; na madirisha yalikuwako, pande zote upande wa ndani, tena palikuwa na mitende juu ya kila mwimo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa matundu madogomadogo kwenye miimo ya inje ya vyumba vyote na hata kwenye kuta zilizotenganisha vyumba. Kulikuwa michoro ya miti ya ngazi kwenye miimo ya ndani iliyoelekea baraza la kupitia.