Ezekiel 40:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chumba cha kuingilia na madirisha na matao yake, pia ile mitende iliyochorwa ukutani, vyote vilifanana na vile vya lango la mashariki. Hapo palikuwa na ngazi saba za kupandia kwenye lango, na matao yake yalikuwa mbele yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Madirisha yake, baraza yake na nakshi yake ya mitende vilikuwa na vipimo sawasawa na vile vya lango linaloelekea mashariki. Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na madirisha yake, na matao yake, na mitende yake, kipimo chake ni sawasawa na kipimo cha lango lililoelekea upande wa mashariki; nao hupanda kwa madaraja saba; na matao yake yalikuwa mbele yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chumba cha kuingilia na madirisha na matao yake, pia ile mitende iliyochorwa ukutani, vyote vilifanana na vile vya lango la mashariki. Hapo palikuwa na ngazi saba za kupandia kwenye lango, na matao yake yalikuwa mbele yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Madirisha yake, baraza yake na nakshi yake ya miti ya mitende vilikuwa na vipimo sawasawa na vile vya lango linaloelekea mashariki. Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Madirisha yake, baraza yake na nakshi yake ya miti ya mitende vilikuwa na vipimo sawasawa na vile vya lango linaloelekea mashariki. Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na madirisha yake, na matao yake, na mitende yake, kipimo chake ni sawasawa na kipimo cha lango lililoelekea upande wa mashariki; nao hupanda kwa madaraja saba; na matao yake yalikuwa mbele yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chumba cha kuingilia na madirisha na matao yake, pia ile mitende iliyochorwa ukutani, vyote vilifanana na vile vya lango la mashariki. Hapo palikuwa na ngazi saba za kupandia kwenye lango, na matao yake yalikuwa mbele yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Madirisha yake na ukumbi wake na machoro ya mitende kipimo chao kilikuwa kilekile cha jengo la lango lililoelekea maawioni kwa jua; kwa vipago saba watu wakalipandia, kisha ukumbi wake ulikuwa mbele yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na madirisha yake, na matao yake, na mitende yake, kipimo chake ni sawasawa na kipimo cha lango lililoelekea upande wa mashariki; nao hupanda kwa madaraja saba; na matao yake yalikuwa mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Chumba cha kuingilia na madirisha na nguzo zake, pamoja na ile miti ya ngazi iliyochorwa juu ya ukuta, vyote vilifanana na vile vya mulango wa upande wa mashariki.