Ezekiel 40:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na ngazi saba za kupandia kwenye njia hiyo ya kuingilia na mwishoni mwake kulikuwa na ukumbi uliokuwa mkabala na ua. Kulikuwa na michoro ya mitende kwenye kuta za ndani zilizokuwa mkabala na hiyo njia ya kuingilia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo. Ilikuwa na nakshi za mitende kwenye kuta zilizochomoza kati ya vyumba kila upande.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena palikuwa na madaraja saba ya kulipandia, na matao yake yalikuwa mbele yake; nalo lilikuwa na mitende, mmoja upande huu, na mmoja upande huu, juu ya miimo yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na ngazi saba za kupandia kwenye njia hiyo ya kuingilia na mwishoni mwake kulikuwa na ukumbi uliokuwa mkabala na ua. Kulikuwa na michoro ya mitende kwenye kuta za ndani zilizokuwa mkabala na hiyo njia ya kuingilia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo, ilikuwa na nakshi ya miti ya mitende kwenye kuta zinazogawanya vyumba kila upande.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulikuwa na ngazi saba za kupandia huko, pamoja na baraza yake mkabala nazo. Ilikuwa na nakshi za miti ya mitende kwenye kuta zilizogawanya vyumba kila upande.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena palikuwa na madaraja saba ya kulipandia, na matao yake yalikuwa mbele yake; nalo lilikuwa na mitende, mmoja upande huu, na mmoja upande huu, juu ya miimo yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na ngazi saba za kupandia kwenye njia hiyo ya kuingilia na mwishoni mwake kulikuwa na ukumbi uliokuwa mkabala na ua. Kulikuwa na michoro ya mitende kwenye kuta za ndani zilizokuwa mkabala na hiyo njia ya kuingilia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo palikuwa na vipago saba vya kupapandia, nao ukumbi wake ulikuwa mbele yao, nao ulikuwa na machoro ya mitende kwenye nguzo zake upande wa huku na upande wa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena palikuwa na madaraja saba ya kulipandia, na matao yake yalikuwa mbele yake; nalo lilikuwa na mitende, mmoja upande huu, na mmoja upande huu, juu ya miimo yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa ngazi saba za kupandia kwenye njia hiyo ya kuingilia na kwa mwisho wake kulikuwa baraza iliokuwa inaelekeana na kiwanja. Kulikuwa michoro ya miti ya ngazi kwenye kuta za ndani zilizokuwa mbele ya njia hiyo ya kuingilia.