Ezekiel 40:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vyumba vya walinzi, ukumbi, na kuta zake vilikuwa na ukubwa uleule kama vile vingine; kulikuwa na madirisha pia kandokando ya hiyo njia ya kuingilia na kwenye ukumbi. Ilikuwa na urefu mita 25 na upana mita kumi na mbili u nusu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vyumba vyake, kuta zilizochomoza kati ya vyumba, na ukumbi wake vyote vilikuwa na vipimo sawa na vile vingine. Hilo lango na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Navyo vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
navyo vyumba vyake vya walinzi, na miimo yake, na matao yake, sawasawa na vipimo hivyo; tena palikuwa na madirisha ndani yake, na katika matao yake pande zote; urefu wake dhiraa hamsini, na upana wake dhiraa ishirini na tano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vyumba vya walinzi, ukumbi, na kuta zake vilikuwa na ukubwa uleule kama vile vingine; kulikuwa na madirisha pia kandokando ya hiyo njia ya kuingilia na kwenye ukumbi. Ilikuwa na urefu mita 25 na upana mita kumi na mbili u nusu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vyumba vyake, kuta zilizogawanya vyumba na ukumbi wake zilikuwa na vipimo sawasawa na zile nyingine. Hilo lango na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Navyo vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vyumba vyake, kuta zilizogawanya vyumba na ukumbi wake zilikuwa na vipimo sawasawa na zile nyingine. Hilo lango na baraza yake vilikuwa na madirisha pande zote. Navyo vilikuwa na urefu wa dhiraa hamsini na upana wa dhiraa ishirini na tano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
navyo vyumba vyake vya walinzi, na miimo yake, na matao yake, sawasawa na vipimo hivyo; tena palikuwa na madirisha ndani yake, na katika matao yake pande zote; urefu wake dhiraa hamsini, na upana wake dhiraa ishirini na tano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vyumba vya walinzi, ukumbi, na kuta zake vilikuwa na ukubwa uleule kama vile vingine; kulikuwa na madirisha pia kandokando ya hiyo njia ya kuingilia na kwenye ukumbi. Ilikuwa na urefu mita 25 na upana mita kumi na mbili u nusu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vyumba vyake na nguzo zake na ukumbi wake vipimo vyao vilikuwa vilevile. Hata madirisha yalilizunguka hilo jengo la lango na ukumbi wake pande zote; nao urefu ulikuwa mikono hamsini, nao upana ulikuwa mikono ishirini na mitano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
navyo vyumba vyake vya walinzi, na miimo yake, na matao yake, sawasawa na vipimo hivyo; tena palikuwa na madirisha ndani yake, na katika matao yake pande zote; urefu wake dhiraa hamsini, na upana wake dhiraa ishirini na tano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vyumba vya walinzi, baraza, na kuta zake vilikuwa na ukubwa ule ule kama vile vingine; kulikuwa vilevile madirisha kandokando ya hiyo njia ya kuingilia na kwenye baraza. Ilikuwa na urefu metre makumi mbili na tano na upana metre kumi na mbili na nusu.