Ezekiel 40:37 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ule ukumbi wa kuingilia ulikuwa mkabala na ua wa nje; kulikuwa na mitende imechorwa kwenye kuta za hiyo nafasi ya kupitia. Pia kulikuwa na ngazi nane za kupandia kuelekea kwenye lango hili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje; miimo yake ilinakshiwa mitende pande zote, na kulikuwa na ngazi nane za kupandia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na miimo yake iliuelekea ua wa nje; na mitende ilikuwa juu ya miimo yake, upande huu na upande huu; tena palikuwa na madaraja manane ya kuupandia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ule ukumbi wa kuingilia ulikuwa mkabala na ua wa nje; kulikuwa na mitende imechorwa kwenye kuta za hiyo nafasi ya kupitia. Pia kulikuwa na ngazi nane za kupandia kuelekea kwenye lango hili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende pande zote, kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baraza yake ilielekeana na ukumbi wa nje, miimo yake ilinakshiwa miti ya mitende pande zote, kulikuwa na ngazi nane za kupandia huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na miimo yake iliuelekea ua wa nje; na mitende ilikuwa juu ya miimo yake, upande huu na upande huu; tena palikuwa na madaraja manane ya kuupandia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ule ukumbi wa kuingilia ulikuwa mkabala na ua wa nje; kulikuwa na mitende imechorwa kwenye kuta za hiyo nafasi ya kupitia. Pia kulikuwa na ngazi nane za kupandia kuelekea kwenye lango hili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukumbi wake uliuelekea ua wa nje, nayo machoro ya mitende yalikuwa penye nguzo zake upande wa huku na wa huko, napo hapo palikuwa na vipago vinane vya kupapandia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na miimo yake iliuelekea ua wa nje; na mitende ilikuwa juu ya miimo yake, upande huu na upande huu; tena palikuwa na madaraja manane ya kuupandia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ile baraza ya kuingilia ilikuwa inaelekea kwenye kiwanja cha inje; kulikuwa miti ya ngazi iliyochorwa kwenye kuta za hiyo nafasi ya kupitia. Kulikuwa vilevile ngazi nane za kupandia kuelekea kwenye mulango huu.