Ezekiel 40:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akaniambia: “Wewe mtu! Tazama vizuri na kusikiliza kwa makini. Zingatia kwa moyo uone kila kitu nitakachokuonesha maana umeletwa hapa ili nikuoneshe kitu. Unapaswa kuwatangazia watu wa Israeli kila kitu utakachoona.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu huyo akaniambia, “Mwanadamu, fungua macho yako uone, na utege masikio yako usikie, nawe uzingatie yote nitakayokuonesha, kwa kuwa ndiyo sababu umeletwa hapa. Iambie nyumba ya Israeli kila kitu utakachoona.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu yule akaniambia, Mwanadamu, tazama kwa macho yako, sikia kwa masikio yako, ukaweke moyoni mwako, yote nitakayokuonyesha; maana umeletwa hapa kusudi nikuonyeshe haya; tangaza habari ya yote utakayoyaona kwa nyumba ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akaniambia: “Wewe mtu! Tazama vizuri na kusikiliza kwa makini. Zingatia kwa moyo uone kila kitu nitakachokuonesha maana umeletwa hapa ili nikuoneshe kitu. Unapaswa kuwatangazia watu wa Israeli kila kitu utakachoona.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu huyo akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa macho yako na usikie kwa masikio yako nawe uzingatie kitu nitakachokuonyesha, kwa kuwa ndiyo sababu umeletwa hapa. Iambie nyumba ya Israeli kila kitu utakachoona.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu huyo akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa macho yako na usikie kwa masikio yako nawe uzingatie kitu nitakachokuonyesha, kwa kuwa ndiyo sababu umeletwa hapa. Iambie nyumba ya Israeli kila kitu utakachoona.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu yule akaniambia, Mwanadamu, tazama kwa macho yako, sikia kwa masikio yako, ukaweke moyoni mwako, yote nitakayokuonesha; maana umeletwa hapa kusudi nikuoneshe haya; tangaza habari ya yote utakayoyaona kwa nyumba ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akaniambia: “Wewe mtu! Tazama vizuri na kusikiliza kwa makini. Zingatia kwa moyo uone kila kitu nitakachokuonesha maana umeletwa hapa ili nikuoneshe kitu. Unapaswa kuwatangazia watu wa Israeli kila kitu utakachoona.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia yule mtu: Mwana wa mtu, tazama kwa macho yako, tena sikiliza kwa masikio yako! Nao moyo wako uuelekeze kuyaangalia yote, nitakayokuonyesha! Kwani umeletwa huku, kusudi uonyeshwe mambo; yote, utakayoyaona huku, uwatangazie walio ukoo wa Isiraeli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu yule akaniambia, Mwanadamu, tazama kwa macho yako, sikia kwa masikio yako, ukaweke moyoni mwako, yote nitakayokuonyesha; maana umeletwa hapa kusudi nikuonyeshe haya; tangaza habari ya yote utakayoyaona kwa nyumba ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, akaniambia hivi: Wewe mwanadamu! Angalia vizuri na kusikiliza kwa uangalifu. Shika kwa moyo uone kila kitu nitakachokuonyesha maana umeletwa hapa kusudi nikuonyeshe kitu. Unapaswa kuwatangazia watu wa Israeli kila kitu utakachoona.