Ezekiel 40:46 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na chumba kinachoelekea kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wanaohudumu madhabahuni. Makuhani hawa ni wale wa ukoo wa Sadoki, ndio hao kati ya watu wa kabila la Lawi wanaoruhusiwa kwenda mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nacho chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wenye usimamizi wa madhabahuni. Hawa ni wana wa Sadoki, ambao ndio Walawi pekee wanaoweza kumkaribia Mwenyezi Mungu ili kuhudumu mbele zake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nacho chumba kinachokabili upande wa kaskazini ni kwa makuhani, walinzi wa malindo ya madhabahu; hao ni wana wa Sadoki, ambao miongoni mwa wana wa Lawi wamkaribia Bwana, ili kumtumikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na chumba kinachoelekea kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wanaohudumu madhabahuni. Makuhani hawa ni wale wa ukoo wa Sadoki, ndio hao kati ya watu wa kabila la Lawi wanaoruhusiwa kwenda mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nacho chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wenye usimamizi wa madhabahuni. Hawa ni wana wa Sadoki, ambao ndio Walawi pekee wanaoweza kumkaribia BWANA ili kuhudumu mbele zake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nacho chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wenye usimamizi wa madhabahuni. Hawa ni wana wa Sadoki, ambao ndio Walawi pekee wanaoweza kumkaribia bwana ili kuhudumu mbele zake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nacho chumba kinachokabili upande wa kaskazini ni cha makuhani, wasimamizi wa madhabahu; hao ni wana wa Sadoki, ambao kati ya wana wa Lawi, ndio waliomkaribia BWANA, ili kumtumikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na chumba kinachoelekea kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wanaohudumu madhabahuni. Makuhani hawa ni wale wa ukoo wa Sadoki, ndio hao kati ya watu wa kabila la Lawi wanaoruhusiwa kwenda mbele ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho chumba kinachoelekea kaskazini ni cha watambikaji wanaongoja zamu mezani pa kutambikia, ndio wana wa Sadoki, ndio wanaomkaribia Bwana peke yao katika wana wa Lawi, wamtumikie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nacho chumba kinachokabili upande wa kaskazini ni kwa makuhani, walinzi wa malindo ya madhabahu; hao ni wana wa Sadoki, ambao miongoni mwa wana wa Lawi wamkaribia BWANA, ili kumtumikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na chumba kinachoelekea upande wa kaskazini ni kwa ajili ya makuhani wanaotumika kwenye mazabahu. Makuhani hawa ni wale wa ukoo wa Zadoki, ndio hao kati ya watu wa kabila la Lawi wanaoruhusiwa kwenda mbele ya Yawe.