Ezekiel 40:48 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, alinipeleka kwenye ukumbi wa kuingilia nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Akalipima lango, nalo lilikuwa na kimo cha mita 2.5 na upana wa mita 7. Na kuta zake zilikuwa na unene mita 1.5 kila upande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akanileta kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nne na kuta zake zilizochomoza zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akanileta mpaka ukumbi wa nyumba, akapima kila mwimo wa ukumbi, dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; na upana wa lango ulikuwa dhiraa tatu upande huu, na dhiraa tatu upande huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, alinipeleka kwenye ukumbi wa kuingilia nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Akalipima lango, nalo lilikuwa na kimo cha mita 2.5 na upana wa mita 7. Na kuta zake zilikuwa na unene mita 1.5 kila upande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akanileta mpaka kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nne na kuta zake zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akanileta mpaka kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nne na kuta zake zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akanileta mpaka ukumbi wa nyumba, akapima kila mwimo wa ukumbi, dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; na upana wa lango ulikuwa dhiraa tatu upande huu, na dhiraa tatu upande huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye, alinipeleka kwenye ukumbi wa kuingilia nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Akalipima lango, nalo lilikuwa na kimo cha mita 2.5 na upana wa mita 7. Na kuta zake zilikuwa na unene mita 1.5 kila upande.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akanipeleka penye ukumbi wa Nyumba, akaupima unene wa miimo ya huo ukumbi, ulikuwa mikono mitano upande wa huku, tena mikono mitano upande wa huko, nao upana wa lango ulikuwa mikono kumi na minne, nazo kuta za kando ya jengo la lango upande wa ndani zilikuwa mikono mitatu upande wa huku na mikono mitatu upande wa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akanileta mpaka ukumbi wa nyumba, akapima kila mwimo wa ukumbi, dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; na upana wa lango ulikuwa dhiraa tatu upande huu, na dhiraa tatu upande huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, alinipeleka kwenye baraza la kuingilia ndani ya nyumba ya Yawe. Akapima mulango, nao ulikuwa na kimo cha metre mbili na nusu na upana wa metre saba. Na kuta zake zilikuwa na unene metre moja na nusu kila upande.