Ezekiel 40:49 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na ngazi za kupandia kwenye ukumbi wa chumba cha kuingilia, ambao ulikuwa na upana wa mita 10 na kina cha mita 6. Kulikuwa na nguzo mbili, nguzo moja kila upande wa mlango.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi na moja; karibu na madaraja ambayo waliupandia; tena palikuwa na nguzo karibu na miimo, moja upande huu, na moja upande huu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na ngazi za kupandia kwenye ukumbi wa chumba cha kuingilia, ambao ulikuwa na upana wa mita 10 na kina cha mita 6. Kulikuwa na nguzo mbili, nguzo moja kila upande wa mlango.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi na moja; karibu na madaraja ambayo waliupandia; tena palikuwa na nguzo karibu na miimo, moja upande huu, na moja upande huu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na ngazi za kupandia kwenye ukumbi wa chumba cha kuingilia, ambao ulikuwa na upana wa mita 10 na kina cha mita 6. Kulikuwa na nguzo mbili, nguzo moja kila upande wa mlango.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Urefu wa ukumbi ulikuwa mikono ishirini, nao upana wake mikono kumi na miwili, tena hapo palikuwa na vipago vya kupapandia, tena penye miimo palikuwa na nguzo, moja upande wa huku na moja upande wa huko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi na moja; karibu na madaraja ambayo waliupandia; tena palikuwa na nguzo karibu na miimo, moja upande huu, na moja upande huu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa ngazi za kupandia kwenye baraza la chumba cha kuingilia, ambalo lilikuwa na urefu wa metre kumi na upana metre sita. Kulikuwa nguzo mbili, nguzo moja kila upande wa mulango.