Ezekiel 40:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, huko, niliona hekalu nalo lilikuwa limezungukwa na ukuta upande wa nje. Yule mtu akauchukua ufito wake wa kupimia ambao ulikuwa na urefu wa mita 3, akaupima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na kimo cha mita 3 na unene wa mita 3.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nikaona ukuta uliozunguka eneo lote la Hekalu. Ule ufito wa kupimia uliokuwa mkononi mwa yule mtu ulikuwa na urefu wa dhiraa ndefu sita, dhiraa ndefu ikiwa sawa na dhiraa na nyanda nne. Akaupima ule ukuta; ulikuwa na unene wa dhiraa ndefu sita, na kimo cha dhiraa ndefu sita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na, tazama, kulikuwa na ukuta nje ya nyumba pande zote, na katika mkono wa mtu yule mwanzi wa kupimia, urefu wake dhiraa sita, kila dhiraa, dhiraa na shubiri; basi akaupima upana wa jengo lile, mwanzi mmoja, na urefu wake, mwanzi mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, huko, niliona hekalu nalo lilikuwa limezungukwa na ukuta upande wa nje. Yule mtu akauchukua ufito wake wa kupimia ambao ulikuwa na urefu wa mita 3, akaupima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na kimo cha mita 3 na unene wa mita 3.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nikaona ukuta uliozunguka eneo lote la Hekalu. Ule ufito wa kupimia uliokuwa mkononi mwa yule mtu ulikuwa na urefu wa dhiraa ndefu sita, yaani, dhiraa ndefu ni sawa na dhiraa na nyanda nne, akapima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na unene wa dhiraa ndefu sita na kimo cha dhiraa ndefu sita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nikaona ukuta uliozunguka eneo lote la Hekalu. Ule ufito wa kupimia uliokuwa mkononi mwa yule mtu ulikuwa na urefu wa dhiraa ndefu sita, yaani, dhiraa ndefu ni sawa na dhiraa na nyanda nne, akapima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na unene wa dhiraa ndefu sita na kimo cha dhiraa ndefu sita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na, tazama, kulikuwa na ukuta nje ya nyumba pande zote, na katika mkono wa mtu yule mwanzi wa kupimia, urefu wake dhiraa sita, kila dhiraa, dhiraa na shubiri; basi akaupima upana wa jengo lile, mwanzi mmoja, na urefu wake, mwanzi mmoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, huko, niliona hekalu nalo lilikuwa limezungukwa na ukuta upande wa nje. Yule mtu akauchukua ufito wake wa kupimia ambao ulikuwa na urefu wa mita 3, akaupima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na kimo cha mita 3 na unene wa mita 3.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikaona ukuta wa nje ulioizunguka Nyumba pande zote pia. Nao mwanzi wa kupimia ulikuwa mkononi mwake yule mtu, ulikuwa wa mikono sita kama mkono wa mtu na upana wa shubiri moja; akaupima upana wa ukuta, ulikuwa mwanzi mmoja, nao urefu wake wa kwenda juu ulikuwa mwanzi mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na, tazama, kulikuwa na ukuta nje ya nyumba pande zote, na katika mkono wa mtu yule mwanzi wa kupimia, urefu wake dhiraa sita, kila dhiraa, dhiraa na shubiri; basi akaupima upana wa jengo lile, mwanzi mmoja, na urefu wake, mwanzi mmoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, huko, niliona hekalu nalo lilikuwa limezungukwa na ukuta upande wa inje. Yule mutu akatwaa ufito wake wa kupima ambao ulikuwa na urefu kwenda juu wa metre tatu, akapima ule ukuta. Ukuta huo ulikuwa na kimo cha metre tatu na unene wa metre tatu.