Ezekiel 41:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mtu akapima urefu wa jengo hadi magharibi pamoja na mabaraza yake pande zake zote, nalo lilikuwa na urefu wa mita 50. Chumba cha kuingilia hekaluni, mahali patakatifu, na mahali patakatifu kabisa,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akapima urefu wa jengo lililoelekeana na ua upande wa nyuma wa Hekalu, pamoja na baraza zake kila upande, kwa kipimo cha dhiraa mia moja. Ukumbi mkuu, na mahali patakatifu, pamoja na baraza inayoelekeana na ukumbi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaupima urefu wa jengo lile lililokabili mahali palipotengeka, palipokuwa nyuma yake, na baraza zake upande huu na upande huu, dhiraa mia; na hekalu la ndani, na kumbi za ua;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mtu akapima urefu wa jengo hadi magharibi pamoja na mabaraza yake pande zake zote, nalo lilikuwa na urefu wa mita 50. Chumba cha kuingilia hekaluni, mahali patakatifu, na mahali patakatifu kabisa,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akapima urefu wa jengo linaloelekeana na ua upande wa nyuma wa Hekalu, pamoja na vyumba vyake kila upande, ilikuwa dhiraa mia moja. Mahali Patakatifu pa nje, mahali Patakatifu pa ndani, pamoja na baraza inayoelekeana na ukumbi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akapima urefu wa jengo linaloelekeana na ua upande wa nyuma wa Hekalu, pamoja na vyumba vyake kila upande, ilikuwa dhiraa mia moja. Sehemu takatifu ya nje, sehemu takatifu ya ndani, pamoja na baraza inayoelekeana na ukumbi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaupima urefu wa jengo lile lililokabili mahali palipotengeka, palipokuwa nyuma yake, na baraza zake upande huu na upande huu, dhiraa mia moja; na hekalu la ndani, na kumbi za ua;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mtu akapima urefu wa jengo hadi magharibi pamoja na mabaraza yake pande zake zote, nalo lilikuwa na urefu wa mita 50. Chumba cha kuingilia hekaluni, mahali patakatifu, na mahali patakatifu kabisa,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaupima urefu wa lile jengo lililopaelekea hapo palipokatazwa watu, lililokuwa nyuma yake Nyumba, na baraza zake upande wa huku na upande wa huko, ulikuwa mikono mia. Upande wa ndani wa hiyo Nyumba nazo kumbi za uani
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaupima urefu wa jengo lile lililokabili mahali palipotengeka, palipokuwa nyuma yake, na baraza zake upande huu na upande huu, dhiraa mia; na hekalu la ndani, na kumbi za ua;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mutu akapima urefu wa jengo mpaka magaribi pamoja na mabaraza yake pande zake zote, nalo lilikuwa na urefu wa metre makumi tano. Chumba cha kuingilia katika hekalu, Pahali Patakatifu, na Pahali Patakatifu Sana,