Ezekiel 41:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwenye mlango wa kuingilia ukumbi kulichorwa viumbe vyenye mabawa na mitende, kama ilivyokuwa kwenye kuta. Na kulikuwa na kifuniko cha ubao kikifunika mlango kwa nje kwenye sehemu ya kuingilia ndani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Juu ya hiyo milango ya Patakatifu palinakshiwa makerubi na mitende kama nakshi zilizokuwa kwenye kuta, na kulikuwa na ubao ulioning’inia mbele ya baraza kwa nje.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na milango ya hekalu ilifanyiziwa makerubi na mitende vile vile, kama zile kuta zilivyofanyiziwa; tena palikuwa na boriti nene juu ya uso wa ukumbi, nje.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwenye mlango wa kuingilia ukumbi kulichorwa viumbe vyenye mabawa na mitende, kama ilivyokuwa kwenye kuta. Na kulikuwa na kifuniko cha ubao kikifunika mlango kwa nje kwenye sehemu ya kuingilia ndani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Juu ya hiyo milango ya Patakatifu palinakshiwa makerubi na miti ya mitende kama yale yaliyonakshiwa kwenye kuta na kulikuwa na ubao ulioning'inia mbele ya baraza kwa nje.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Juu ya hiyo milango ya Patakatifu palinakshiwa makerubi na miti ya mitende kama yale yaliyonakshiwa kwenye kuta, na kulikuwa na ubao ulioning’inia mbele ya baraza kwa nje.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na milango ya hekalu ilitengenezwa makerubi na mitende vile vile, kama zile kuta zilivyotengenezwa; tena palikuwa na boriti nene juu ya uso wa ukumbi, nje.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwenye mlango wa kuingilia ukumbi kulichorwa viumbe vyenye mabawa na mitende, kama ilivyokuwa kwenye kuta. Na kulikuwa na kifuniko cha ubao kikifunika mlango kwa nje kwenye sehemu ya kuingilia ndani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo penye milango hii ya Patakatifu palikuwa pamechorwa Makerubi na mitende, kama palivyochorwa kutani. Tena hapo upande wa mbele wa ukumbi wa nje palikuwa na baraza iliyotengenezwa kwa mbao za miti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na milango ya hekalu ilifanyiziwa makerubi na mitende vile vile, kama zile kuta zilivyofanyiziwa; tena palikuwa na boriti nene juu ya uso wa ukumbi, nje.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwenye mulango wa kuingilia kwenye baraza kulichorwa makerubi na miti ya ngazi kama ilivyokuwa kwenye kuta. Na kulikuwa kifuniko cha ubao kikifunika mulango kwa inje kwenye sehemu ya kuingilia ndani.