Ezekiel 41:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akaenda kwenye chumba cha ndani kabisa. Akaipima nafasi iliyoelekea huko, nayo ilikuwa na kimo cha mita 1 na upana mita 3.5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita tatu u nusu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akaingia mahali patakatifu na kupima miimo ya ingilio, kila mmoja ulikuwa na upana wa dhiraa mbili. Ingilio lilikuwa na upana wa dhiraa sita, na kuta zilizochomoza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akaingia ndani, akapima kila mwimo wa maingilio, dhiraa mbili; nayo maingilio, dhiraa sita; na upana wa maingilio dhiraa saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akaenda kwenye chumba cha ndani kabisa. Akaipima nafasi iliyoelekea huko, nayo ilikuwa na kimo cha mita 1 na upana mita 3.5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita tatu u nusu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akaingia sehemu ya ndani ya patakatifu na kupima miimo ya ingilio, kila mmoja ulikuwa na upana wa dhiraa mbili. Ingilio lilikuwa na upana wa dhiraa sita, na kuta zilizotokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akaingia sehemu takatifu ndani ya Hekalu na kupima miimo ya ingilio, kila mmoja ulikuwa na upana wa dhiraa mbili. Ingilio lilikuwa na upana wa dhiraa sita, na kuta zilizotokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akaingia ndani, akapima kila mwimo wa maingilio, dhiraa mbili; nayo maingilio, dhiraa sita; na upana wa maingilio dhiraa saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akaenda kwenye chumba cha ndani kabisa. Akaipima nafasi iliyoelekea huko, nayo ilikuwa na kimo cha mita 1 na upana mita 3.5. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa mita tatu u nusu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaingia chumba cha ndani, akaupima mwimo wa hapo pa kuingia ulikuwa mikono miwili, napo hapo pa kuingia palikuwa mikono sita, nao upana wa kando pa kuingia ulikuwa mikono saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akaingia ndani, akapima kila mwimo wa maingilio, dhiraa mbili; nayo maingilio, dhiraa sita; na upana wa maingilio dhiraa saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akaenda kwenye chumba cha ndani kabisa. Akaipima nafasi iliyoelekea huko, nayo ilikuwa na kimo cha metre moja na upana metre tatu na nusu. Nafasi hiyo ilikuwa na kuta kila upande zenye unene wa metre tatu na nusu.