Ezekiel 41:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akakipima chumba chenyewe, nacho kilikuwa cha mraba pande zake zikiwa na upana wa mita 10. Chumba hiki kilikuwa mbele ya ukumbi wa katikati. Kisha, akaniambia, “Hapa ndipo mahali patakatifu kabisa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akapima urefu wa mahali patakatifu; ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini hadi mwisho wa sehemu ya nje ya ukumbi mkuu. Akaniambia, “Hapa ndipo Patakatifu pa Patakatifu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaupima urefu wake; dhiraa ishirini, na upana wake, dhiraa ishirini, mbele ya hekalu; akaniambia, Hapa ndipo mahali patakatifu kuliko kila mahali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akakipima chumba chenyewe, nacho kilikuwa cha mraba pande zake zikiwa na upana wa mita 10. Chumba hiki kilikuwa mbele ya ukumbi wa katikati. Kisha, akaniambia, “Hapa ndipo mahali patakatifu kabisa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye akapima urefu wa ndani ya patakatifu nao ulikuwa dhiraa ishirini na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini hadi mwisho wa sehemu ya nje ya patakatifu. Akaniambia, “Hapa ndipo Patakatifu pa Patakatifu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye akapima urefu wa sehemu takatifu ndani, nao ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa ishirini hadi mwisho wa sehemu ya nje ya sehemu takatifu. Akaniambia, “Hapa ndipo Patakatifu pa Patakatifu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaupima urefu wake; dhiraa ishirini, na upana wake, dhiraa ishirini, mbele ya hekalu; akaniambia, Hapa ndipo mahali patakatifu kuliko kila mahali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akakipima chumba chenyewe, nacho kilikuwa cha mraba pande zake zikiwa na upana wa mita 10. Chumba hiki kilikuwa mbele ya ukumbi wa katikati. Kisha, akaniambia, “Hapa ndipo mahali patakatifu kabisa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaupima urefu wake, ulikuwa mikono ishirini, nao upana ulikuwa mikono ishirini, kama upande wa mbele wa Patakatifu ulivyokuwa. Akaniambia; Hapa ndipo Patakatifu Penyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaupima urefu wake; dhiraa ishirini, na upana wake, dhiraa ishirini, mbele ya hekalu; akaniambia, Hapa ndipo mahali patakatifu kuliko kila mahali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akakipima chumba chenyewe, nacho kilikuwa cha muraba pande zake zikiwa na upana wa metre kumi. Chumba hiki kilikuwa mbele ya baraza la katikati. Kisha, akaniambia: Hapa ndipo Pahali Patakatifu Sana.