Ezekiel 41:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vyumba hivi, vilikuwa katika majengo ya ghorofa tatu, na kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Ukuta wa nje wa hekalu kila kwenye ghorofa ulikuwa mwembamba kuliko ule wa ghorofa ya chini, ili vile vyumba viwe imara bila ya kuutegemea ukuta wa hekalu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vyumba vya pembeni vilikuwa na ghorofa tatu, kimoja juu ya kingine, kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Kulikuwa na boriti katika ukuta wote wa Hekalu ili kuimarisha vyumba vya pembeni; kwa hiyo boriti hizo hazikushikamanishwa kwenye ukuta wa Hekalu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na vile vyumba vya mbavuni vilikuwa na orofa tatu, moja juu ya mwenziwe; vilikuwa thelathini, safu baada ya safu; navyo viliingia ndani ya ukuta uliokuwa wa nyumba, kwa vile vyumba vya mbavuni pande zote vipate kushikamana nao, wala visishikamane na ukuta wa nyumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vyumba hivi, vilikuwa katika majengo ya ghorofa tatu, na kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Ukuta wa nje wa hekalu kila kwenye ghorofa ulikuwa mwembamba kuliko ule wa ghorofa ya chini, ili vile vyumba viwe imara bila ya kuutegemea ukuta wa hekalu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vyumba vya pembeni vilikuwa na ghorofa tatu, kimoja juu ya kingine, kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Kulikuwa na boriti katika ukuta wote wa Hekalu ili kuimarisha vyumba vya pembeni, kwa hiyo boriti hizo hazikushikamanishwa kwenye ukuta wa Hekalu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vyumba vya pembeni vilikuwa na ghorofa tatu, kimoja juu ya kingine, kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Kulikuwa na boriti katika ukuta wote wa Hekalu ili kuimarisha vyumba vya pembeni, kwa hiyo boriti hizo hazikushikamanishwa kwenye ukuta wa Hekalu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vile vyumba vya mbavuni vilikuwa na ghorofa tatu, moja juu ya mwenziwe; vilikuwa thelathini, safu baada ya safu; navyo viliingia ndani ya ukuta uliokuwa wa nyumba, kwa vile vyumba vya mbavuni pande zote vipate kushikamana nao, wala visishikamane na ukuta wa nyumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vyumba hivi, vilikuwa katika majengo ya ghorofa tatu, na kila ghorofa ilikuwa na vyumba thelathini. Ukuta wa nje wa hekalu kila kwenye ghorofa ulikuwa mwembamba kuliko ule wa ghorofa ya chini, ili vile vyumba viwe imara bila ya kuutegemea ukuta wa hekalu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo vyumba vya kando vilikuwa vitatu kwenda juu, kila kimoja juu ya kingine, tena vilikuwa kila mara thelathini kwenda mbele vikizunguka ukutani penye Nyumba kando, vipate kushikizwa humo, lakini havikushukizwa ndani ya ukuta wa Nyumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na vile vyumba vya mbavuni vilikuwa na orofa tatu, moja juu ya mwenziwe; vilikuwa thelathini, safu baada ya safu; navyo viliingia ndani ya ukuta uliokuwa wa nyumba, kwa vile vyumba vya mbavuni pande zote vipate kushikamana nao, wala visishikamane na ukuta wa nyumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vyumba hivi vilikuwa katika majengo ya gorofi tatu, na kila gorofi ilikuwa na vyumba makumi tatu. Ukuta wa inje wa hekalu kila kwenye gorofi ulikuwa mwembamba kuliko ule wa gorofi ya chini, kusudi vile vyumba vikuwe imara bila kuutegemea ukuta wa hekalu.