Ezekiel 41:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa upande, zile kuta za hekalu zikitazamwa kutokea nje, zilionekana kuwa na unene uleule toka chini hadi juu. Mkabala na ukuta wa nje wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nje ya vyumba, kulikuwa na ngazi mbili, ambazo zilifanya iwe rahisi kwenda juu kutokea ghorofa ya chini hadi ile ya juu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vyumba vya pembeni vilivyozunguka Hekalu vilizidi kupanuka kulingana na sakafu zilivyoenda juu. Ujenzi uliozunguka Hekalu ulijengwa kukwea juu, kwa hiyo vyumba vilipanuka kwa kadiri ya kila kimoja kilivyoenda juu. Ngazi za kupandia zilianzia sakafu ya chini hadi sakafu ya juu kabisa kupitia kwa sakafu ya kati.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na vile vyumba vya mbavuni vilizidi kuwa vipana, kwa kadiri vilivyoizunguka nyumba juu kwa juu; maana kule kuzunguka kwake kulikwenda juu kwa juu, kuizunguka nyumba; basi upana wa nyumba ulikuwa ule ule hata juu; basi hupanda juu toka chumba cha chini hata chumba cha juu, kwa njia ya kile chumba cha katikati.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa upande, zile kuta za hekalu zikitazamwa kutokea nje, zilionekana kuwa na unene uleule toka chini hadi juu. Mkabala na ukuta wa nje wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nje ya vyumba, kulikuwa na ngazi mbili, ambazo zilifanya iwe rahisi kwenda juu kutokea ghorofa ya chini hadi ile ya juu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vyumba vya pembeni vilivyozunguka Hekalu vilizidi kupanuka kulingana na sakafu zilivyokwenda juu. Ujenzi uliozunguka Hekalu ulijengwa kukwea juu, kwa hiyo vyumba vilipanuka kwa kadiri ya kila kimoja kilivyokwenda juu. Ngazi za kupandia zilianzia sakafu ya chini hadi sakafu ya juu kabisa kwa kupitia sakafu ya kati.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vyumba vya pembeni vilivyozunguka Hekalu vilizidi kupanuka kulingana na sakafu zilivyokwenda juu. Ujenzi uliozunguka Hekalu ulijengwa kukwea juu, kwa hiyo vyumba vilipanuka kwa kadiri ya kila kimoja kilivyokwenda juu. Ngazi za kupandia zilianzia sakafu ya chini hadi sakafu ya juu kabisa kwa kupitia sakafu ya kati.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na vile vyumba vya mbavuni vilizidi kuwa vipana, kwa kadiri vilivyoizunguka nyumba juu kwa juu; maana kule kuzunguka kwake kulikwenda juu kwa juu, kuizunguka nyumba; basi upana wa nyumba ulikuwa ule ule hadi juu; basi hupanda juu toka chumba cha chini hadi chumba cha juu, kwa njia ya kile chumba cha katikati.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa upande, zile kuta za hekalu zikitazamwa kutokea nje, zilionekana kuwa na unene uleule toka chini hadi juu. Mkabala na ukuta wa nje wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nje ya vyumba, kulikuwa na ngazi mbili, ambazo zilifanya iwe rahisi kwenda juu kutokea ghorofa ya chini hadi ile ya juu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo vyumba vya kando vilivyozunguka kila dari lao la juu viliongezwa kuwa vipana kuliko vya chini; kwa kuzunguka hivyo nayo Nyumba yenyewe, ulipoitazama nje, upande wake wa juu ulikwenda ukiongezwa pande zake zote. Mtu alipotaka kupandia vyumba vya juu alitoka penye vyumba vya chini, akapita penye vile vya kati, afike juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na vile vyumba vya mbavuni vilizidi kuwa vipana, kwa kadiri vilivyoizunguka nyumba juu kwa juu; maana kule kuzunguka kwake kulikwenda juu kwa juu, kuizunguka nyumba; basi upana wa nyumba ulikuwa ule ule hata juu; basi hupanda juu toka chumba cha chini hata chumba cha juu, kwa njia ya kile chumba cha katikati.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa upande, zile kuta za hekalu zikitazamwa kutokea inje, zilionekana kuwa na unene uleule toka chini mpaka juu. Kuelekea ukuta wa inje wa nyumba ya Yawe, inje ya vyumba, kulikuwa ngazi mbili, ambazo zilifanya ikuwe vyepesi kwenda juu kutokea gorofi ya chini mpaka ile ya juu.