Ezekiel 42:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mtu akaniambia, “Vyumba hivi vyote ni vitakatifu. Ndani ya vyumba hivi makuhani wanaoingia mbele ya Mwenyezi-Mungu, wanakula sadaka takatifu kabisa: Tambiko takatifu kabisa na humo ndimo mnamowekwa sadaka za nafaka, sadaka za kuondoa dhambi na sadaka za kuondoa hatia kwa kuwa mahali hapo ni patakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akaniambia, “Vyumba vya upande wa kaskazini na vya upande wa kusini, ambavyo vinaelekeana na ukumbi wa Hekalu, ni vyumba vya makuhani, ambako wale makuhani ambao humkaribia Mwenyezi Mungu watakulia zile sadaka takatifu sana. Huko ndiko wataziweka zile sadaka takatifu sana, yaani sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia, kwa kuwa mahali hapo ni patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akaniambia, Vyumba vya upande wa kaskazini, na vyumba vya upande wa kusini, ambavyo vyaelekea mahali palipotengeka, ni vyumba vitakatifu; humo makuhani, wamkaribiao Bwana, watakula vitu vilivyo vitakatifu sana; humo wataviweka vitu vilivyo vitakatifu sana, na sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia; kwa maana mahali hapo ni patakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mtu akaniambia, “Vyumba hivi vyote ni vitakatifu. Ndani ya vyumba hivi makuhani wanaoingia mbele ya Mwenyezi-Mungu, wanakula sadaka takatifu kabisa: tambiko takatifu kabisa na humo ndimo mnamowekwa sadaka za nafaka, sadaka za kuondoa dhambi na sadaka za kuondoa hatia kwa kuwa mahali hapo ni patakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akaniambia, “Vyumba vya upande wa kaskazini na vya upande wa kusini ambavyo vinaelekeana na ukumbi wa Hekalu ni vyumba vya makuhani, mahali ambapo wale makuhani ambao humkaribia BWANA watakula zile sadaka takatifu sana. Huko ndiko watakakoweka zile sadaka takatifu sana, yaani, sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia, kwa kuwa mahali ni patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akaniambia, “Vyumba vya upande wa kaskazini na vya upande wa kusini ambavyo vinaelekeana na ukumbi wa Hekalu ni vyumba vya makuhani, mahali ambapo wale makuhani ambao humkaribia bwana watakula zile sadaka takatifu sana. Huko ndiko watakakoweka zile sadaka takatifu sana, yaani, sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia, kwa kuwa mahali ni patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akaniambia, Vyumba vya upande wa kaskazini, na vyumba vya upande wa kusini, ambavyo vyaelekea mahali palipotengeka, ni vyumba vitakatifu; humo makuhani, wamkaribiao BWANA, watakula vitu vilivyo vitakatifu sana; humo wataviweka vitu vilivyo vitakatifu sana, na sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia; kwa maana mahali hapo ni patakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mtu akaniambia, “Vyumba hivi vyote ni vitakatifu. Ndani ya vyumba hivi makuhani wanaoingia mbele ya Mwenyezi-Mungu, wanakula sadaka takatifu kabisa: Tambiko takatifu kabisa na humo ndimo mnamowekwa sadaka za nafaka, sadaka za kuondoa dhambi na sadaka za kuondoa hatia kwa kuwa mahali hapo ni patakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaniambia: Vyumba vya upande wa kaskazini, hata vyumba vya upande wa kusini vilivyopaelekea palipokatazwa watu, ndivyo vyumba vitakatifu; ndimo, watambikaji watakamokula vyakula vitakatifu vyenyewe, tena ndimo, watakamoviweka vipaji vitakatifu vyenyewe, vilaji vya tambiko na nyama za ng'ombe za tambiko za weuo nazo zao za upozi, kwani ndivyo vyumba vitakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akaniambia, Vyumba vya upande wa kaskazini, na vyumba vya upande wa kusini, ambavyo vyaelekea mahali palipotengeka, ni vyumba vitakatifu; humo makuhani, wamkaribiao BWANA, watakula vitu vilivyo vitakatifu sana; humo wataviweka vitu vilivyo vitakatifu sana, na sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia; kwa maana mahali hapo ni patakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mutu akaniambia: Vyumba hivi vyote ni vitakatifu. Ndani ya vyumba hivi makuhani wanaoingia mbele ya Yawe, wanakula sadaka takatifu kabisa: sadaka takatifu kabisa na humo ndimo munamowekwa sadaka za vyakula, sadaka za kuomba kusamehewa zambi na sadaka kwa ajili ya malipo ya kosa kwa sababu pahali hapo ni patakatifu.