Ezekiel 42:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani ambao watakuwa wamehudumu katika patakatifu, wanapotaka kwenda kwenye ua wa nje, ni lazima wayaache humo mavazi waliyovaa walipokuwa wanahudumu mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa sababu mavazi hayo ni matakatifu. Ni lazima wavae mavazi mengine kabla ya kutoka nje ambako watu wanakusanyika.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara makuhani waingiapo mahali patakatifu, hawaruhusiwi kwenda kwenye ukumbi wa nje hadi wayaache mavazi ambayo walivaa wakiwa wanahudumu, kwa kuwa hayo mavazi ni matakatifu. Inawapasa kuvaa mavazi mengine kabla hawajakaribia eneo lililo wazi kwa ajili ya watu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Makuhani watakapoingia ndani, hawatatoka mahali patakatifu kwenda hata ua wa nje; lakini wataweka mavazi yao katika mahali wahudumiapo; maana ni matakatifu; nao watavaa mavazi mengine, na kupakaribia mahali palipo mahali pa watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani ambao watakuwa wamehudumu katika patakatifu, wanapotaka kwenda kwenye ua wa nje, ni lazima wayaache humo mavazi waliyovaa walipokuwa wanahudumu mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa sababu mavazi hayo ni matakatifu. Ni lazima wavae mavazi mengine kabla ya kutoka nje ambako watu wanakusanyika.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara makuhani waingiapo mahali patakatifu, hawaruhusiwi kwenda kwenye ukumbi wa nje mpaka wayaache mavazi ambayo walivaa wakiwa wanahudumu, kwa kuwa hayo mavazi ni matakatifu. Inawapasa kuvaa mavazi mengine kabla hawajakaribia eneo lililo wazi kwa ajili ya watu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara makuhani waingiapo mahali patakatifu, hawaruhusiwi kwenda kwenye ukumbi wa nje mpaka wayaache mavazi ambayo walivaa wakiwa wanahudumu, kwa kuwa hayo mavazi ni matakatifu. Inawapasa kuvaa mavazi mengine kabla hawajakaribia eneo lililo wazi kwa ajili ya watu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makuhani watakapoingia ndani, hawatatoka mahali patakatifu kwenda hadi katika ua wa nje; lakini wataweka mavazi yao katika mahali wahudumiapo; maana ni matakatifu; nao watavaa mavazi mengine, na kupakaribia mahali pa wazi kwa watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani ambao watakuwa wamehudumu katika patakatifu, wanapotaka kwenda kwenye ua wa nje, ni lazima wayaache humo mavazi waliyovaa walipokuwa wanahudumu mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa sababu mavazi hayo ni matakatifu. Ni lazima wavae mavazi mengine kabla ya kutoka nje ambako watu wanakusanyika.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watambikaji wakitaka kuingia humo, wasitoke Patakatifu na kupitia penye ua wa nje! Humo ndimo, wayaweke mavazi yao waliyoyavaa wakimtumikia Mungu, kwani nayo ni matakatifu. Sharti wavae mavazi mengine, kisha wapakaribie, watu walipo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Makuhani watakapoingia ndani, hawatatoka mahali patakatifu kwenda hata ua wa nje; lakini wataweka mavazi yao katika mahali wahudumiapo; maana ni matakatifu; nao watavaa mavazi mengine, na kupakaribia mahali palipo mahali pa watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makuhani ambao watakuwa wakitumika katika Pahali Patakatifu, wanapotaka kwenda kwenye kiwanja cha inje, ni lazima waache humo nguo zao walizovaa walipokuwa wanatumika mbele ya Yawe kwa sababu nguo hizo ni takatifu. Ni lazima wavae nguo zingine mbele ya kutoka inje ambako watu wanakusanyika.