Ezekiel 43:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale makuhani walio wa kabila la Lawi ambao ni wazawa wa Sadoki, ndio tu watakaonikaribia ili kunihudumia. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Utawapa fahali mchanga kuwa sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi kwa makuhani, ambao ni Walawi, wa jamaa ya Sadoki, ndio watakaonikaribia kuhudumu mbele zangu, asema Bwana Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utawapa makuhani Walawi, walio wa uzao wa Sadoki, walio karibu nami, ili kunihudumu, asema Bwana MUNGU, ng'ombe mume mchanga awe sadaka ya dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale makuhani walio wa kabila la Lawi ambao ni wazawa wa Sadoki, ndio tu watakaonikaribia ili kunihudumia. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Utawapa fahali mchanga kuwa sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi kwa makuhani, ambao ni Walawi, wa jamaa ya Sadoki, ndio watakaonikaribia kuhudumu mbele zangu, asema BWANA Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi kwa makuhani, ambao ni Walawi, wa jamaa ya Sadoki, ndio watakaonikaribia kuhudumu mbele zangu, asema bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utawapa makuhani Walawi, walio wa uzao wa Sadoki, walio karibu nami, ili kunihudumu, asema Bwana MUNGU, ng'ombe dume mchanga awe sadaka ya dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale makuhani walio wa kabila la Lawi ambao ni wazawa wa Sadoki, ndio tu watakaonikaribia ili kunihudumia. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Utawapa fahali mchanga kuwa sadaka ya kuondoa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, utakapotoa ndama ya ng'ombe ya kiume kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo, uwape watambikaji wa Kilawi walio wa uzao wa Sadoki, maana ndio wanaonikaribia na kunitumikia; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utawapa makuhani Walawi, walio wa uzao wa Sadoki, walio karibu nami, ili kunihudumu, asema Bwana MUNGU, ng’ombe mume mchanga awe sadaka ya dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale makuhani wanaokuwa wa kabila la Lawi ambao ni wazao wa Zadoki, ndio tu watakaokaribia mbele yangu kwa kunitumikia. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.– Utawapa ngombe dume muchanga kuwa sadaka ya kusamehewa zambi.