Ezekiel 43:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utatwaa damu yake na kuitia juu ya pembe nne za madhabahu na juu ya ncha nne za daraja na juu ya pambizo yake pande zote. Hivyo ndivyo utakavyoitakasa madhabahu na kuiweka wakfu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Itakupasa kuchukua sehemu ya hiyo damu ya mnyama huyo, na kuiweka juu ya hizo pembe nne za madhabahu, na juu ya ncha zake nne za sehemu ya juu kuzunguka ukingo wote, ili kuitakasa madhabahu, na kufanya upatanisho kwa ajili yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe utatwaa baadhi ya damu yake, na kuitia juu ya pembe zake nne, na juu ya ncha nne za daraja, na juu ya pambizo yake pande zote; ndivyo utakavyoitakasa, na kuifanyia upatanisho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utatwaa damu yake na kuitia juu ya pembe nne za madhabahu na juu ya ncha nne za daraja na juu ya pambizo yake pande zote. Hivyo ndivyo utakavyoitakasa madhabahu na kuiweka wakfu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Itakupasa kuchukua baadhi ya hiyo damu ya mnyama huyo na kuiweka juu ya hizo pembe nne za madhabahu na juu ya ncha zake nne za sehemu ya juu kuzunguka ukingo wote, ili kuitakasa madhabahu na kufanya upatanisho kwa ajili yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Itakupasa kuchukua baadhi ya hiyo damu ya mnyama huyo na kuiweka juu ya hizo pembe nne za madhabahu na juu ya ncha zake nne za sehemu ya juu kuzunguka ukingo wote, ili kuitakasa madhabahu na kufanya upatanisho kwa ajili yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe utatwaa baadhi ya damu yake, na kuitia juu ya pembe zake nne, na juu ya ncha nne za daraja, na juu ya pambizo yake pande zote; ndivyo utakavyoitakasa, na kuifanyia upatanisho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utatwaa damu yake na kuitia juu ya pembe nne za madhabahu na juu ya ncha nne za daraja na juu ya pambizo yake pande zote. Hivyo ndivyo utakavyoitakasa madhabahu na kuiweka wakfu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha sharti uchote damu katika damu yake, uinyunyizie pembe zake nne napo penye zile pembe nne za daraja napo penye kitalu kipazungukacho! Ndivyo, utakavyopaeua pamoja na kupapatia upozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe utatwaa baadhi ya damu yake, na kuitia juu ya pembe zake nne, na juu ya ncha nne za daraja, na juu ya pambizo yake pande zote; ndivyo utakavyoitakasa, na kuifanyia upatanisho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utatwaa damu yake na kuitia juu ya pembe ine za mazabahu na juu ya chongo ine za daraja na juu ya muzunguko wake pande zote. Hivyo ndivyo utakavyoisafisha mazabahu na kuitakasa.