Ezekiel 44:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kwa sababu waliongoza ibada za miungu kwa ajili ya watu wa Israeli, wakawafanya watu kutenda dhambi, basi, nimeunyosha mkono wangu kuwaadhibu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Nao watabeba adhabu yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kwa sababu walitumikia watu wakiwa mbele ya sanamu zao, na kuifanya nyumba ya Israeli ianguke kwenye dhambi, kwa hiyo nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba ni lazima wachukue matokeo ya dhambi yao, asema Bwana Mungu Mwenyezi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu waliwahudumia mbele ya vinyago vyao, wakawa kwazo la uovu kwa nyumba ya Israeli; basi nimeuinua mkono wangu juu yao, asema Bwana MUNGU, nao watachukua uovu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kwa sababu waliongoza ibada za miungu kwa ajili ya watu wa Israeli, wakawafanya watu kutenda dhambi, basi, nimeunyosha mkono wangu kuwaadhibu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Nao watabeba adhabu yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kwa sababu waliwatumikia watu mbele ya sanamu zao na kuifanya nyumba ya Israeli ianguke kwenye dhambi, kwa hiyo nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba ni lazima wachukue matokeo ya dhambi yao, asema BWANA Mwenyezi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kwa sababu waliwatumikia watu mbele ya sanamu zao na kuifanya nyumba ya Israeli ianguke kwenye dhambi, kwa hiyo nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba ni lazima wachukue matokeo ya dhambi yao, asema bwana Mwenyezi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu waliwahudumia mbele ya vinyago vyao, wakawa kwazo la uovu kwa nyumba ya Israeli; basi nimeuinua mkono wangu juu yao, asema Bwana MUNGU, nao watachukua uovu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kwa sababu waliongoza ibada za miungu kwa ajili ya watu wa Israeli, wakawafanya watu kutenda dhambi, basi, nimeunyosha mkono wangu kuwaadhibu. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Nao watabeba adhabu yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa waliwatumikia watu mbele ya magogo yao ya kutambikia, wakawakosesha hivyo walio mlango wa Isiraeli, wakore manza, kwa sababu hii nimewaapia kwa kuuinua mkono wangu kwamba: Watatwikwa manza zao, walizozikora; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu waliwahudumia mbele ya vinyago vyao, wakawa kwazo la uovu kwa nyumba ya Israeli; basi nimeuinua mkono wangu juu yao, asema Bwana MUNGU, nao watachukua uovu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa sababu waliongoza ibada za miungu kwa ajili ya watu wa Israeli, wakasukuma watu kutenda zambi, basi, nimeunyoosha mukono wangu kuwaazibu. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe.– Nao watabeba azabu yao.