Ezekiel 44:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watakapotoka kwenda kwenye ua wa nje kwa watu, watavua mavazi waliyovaa wakati walipokuwa wanahudumu na kuyaweka katika vyumba vitakatifu. Ni lazima wavae mavazi mengine, ili watu wasije wakawa najisi kwa kugusa mavazi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watakapotoka ili kuingia katika ukumbi wa nje mahali watu walipo, watavua nguo walizokuwa wakihudumu nazo na wataziacha katika vyumba vitakatifu nao watavaa nguo nyingine, ili wasije wakaambukiza watu utakatifu kupitia mavazi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watakapotoka kuingia ua wa nje, yaani, ua wa nje wa watu, ndipo watakapoyavua mavazi yao waliyovaa katika huduma yao, na kuyaweka katika vile vyumba vitakatifu, nao watavaa mavazi mengine, wasije wakawatakasa watu kwa mavazi yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watakapotoka kwenda kwenye ua wa nje kwa watu, watavua mavazi waliyovaa wakati walipokuwa wanahudumu na kuyaweka katika vyumba vitakatifu. Ni lazima wavae mavazi mengine, ili watu wasije wakawa najisi kwa kugusa mavazi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watakapotoka ili kuingia katika ukumbi wa nje mahali watu walipo, watavua nguo walizokuwa wakihudumu nazo na wataziacha katika vyumba vitakatifu nao watavaa nguo nyingine, ili kwamba wasije wakaambukiza watu utakatifu kwa njia ya mavazi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watakapotoka ili kuingia katika ukumbi wa nje mahali watu walipo, watavua nguo walizokuwa wakihudumu nazo na wataziacha katika vyumba vitakatifu nao watavaa nguo nyingine, ili kwamba wasije wakaambukiza watu utakatifu kwa njia ya mavazi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watakapotoka kuingia ua wa nje, yaani, ua wa nje wa watu, ndipo watakapoyavua mavazi yao waliyovaa katika huduma yao, na kuyaweka katika vile vyumba vitakatifu, nao watavaa mavazi mengine, wasije wakawatakasa watu kwa mavazi yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watakapotoka kwenda kwenye ua wa nje kwa watu, watavua mavazi waliyovaa wakati walipokuwa wanahudumu na kuyaweka katika vyumba vitakatifu. Ni lazima wavae mavazi mengine, ili watu wasije wakawa najisi kwa kugusa mavazi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watakapotoka kwenda katika ua wa nje, ni ule ua wa nje, watu walipo, sharti wayavue mavazi yao, waliyoyavaa wakifanya kazi za utumishi, wayaweke katika vile vyumba vya Patakatifu, kisha wavae mavazi mengine, wasiwapatie watu utakatifu kwa hayo mavazi yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watakapotoka kuingia ua wa nje, yaani, ua wa nje wa watu, ndipo watakapoyavua mavazi yao waliyovaa katika huduma yao, na kuyaweka katika vile vyumba vitakatifu, nao watavaa mavazi mengine, wasije wakawatakasa watu kwa mavazi yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watakapotoka kwenda kwenye kiwanja cha inje kwa watu, watatosha nguo walizovaa wakati walipokuwa wanatumika na kuziweka katika vyumba vitakatifu. Ni lazima wavae nguo zingine, kusudi watu wasijitakase kwa kugusa nguo zao.