Ezekiel 44:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vitu vyote vilivyo bora vya malimbuko yenu na vya matoleo yenu ya kila aina vitakuwa kwa ajili ya makuhani. Tena mtawapa sehemu ya kwanza ya unga wenu, ili mlete baraka juu ya nyumba zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yote yaliyo bora ya malimbuko ya vitu vyote na matoleo yenu maalum vitakuwa vya makuhani. Inawapasa kuwapa malimbuko ya kwanza ya unga wenu ili baraka ipate kuwa katika nyumba zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kitu cha kwanza cha malimbuko yote ya vitu vyote, na kila toleo la kila kitu cha matoleo yenu, litakuwa la makuhani. Tena mtampa kuhani sehemu ya kwanza ya unga mbichi, ili kukalisha baraka juu ya nyumba yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vitu vyote vilivyo bora vya malimbuko yenu na vya matoleo yenu ya kila aina vitakuwa kwa ajili ya makuhani. Tena mtawapa sehemu ya kwanza ya unga wenu, ili mlete baraka juu ya nyumba zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yote yaliyo bora ya malimbuko ya vitu vyote na matoleo yenu maalum vitakuwa vya makuhani. Inawapasa kuwapa malimbuko ya kwanza ya unga wenu ili kwamba baraka ipate kuwa katika nyumba zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yote yaliyo bora ya malimbuko ya vitu vyote na matoleo yenu maalum vitakuwa vya makuhani. Inawapasa kuwapa malimbuko ya kwanza ya unga wenu ili kwamba baraka ipate kuwa katika nyumba zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kitu cha kwanza cha malimbuko yote ya vitu vyote, na kila toleo la kila kitu cha matoleo yenu, litakuwa la makuhani. Tena mtampa kuhani sehemu ya kwanza ya unga mbichi, ili kuleta baraka juu ya nyumba yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vitu vyote vilivyo bora vya malimbuko yenu na vya matoleo yenu ya kila aina vitakuwa kwa ajili ya makuhani. Tena mtawapa sehemu ya kwanza ya unga wenu, ili mlete baraka juu ya nyumba zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo malimbuko yote pia yanayotolewa kwa kuwa ya kwanza, navyo vipaji vyenu vyote vingine, mtakavyovitoa, vitakuwa mali zao watambikaji nao unga wenu wa kwanza wa kupika mikate mtawapa watambikaji, mbaraka izikalie nyumba zenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kitu cha kwanza cha malimbuko yote ya vitu vyote, na kila toleo la kila kitu cha matoleo yenu, litakuwa la makuhani. Tena mtampa kuhani sehemu ya kwanza ya unga mbichi, ili kukalisha baraka juu ya nyumba yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu ya kwanza ya malimbuko yenu na vya matoleo yenu ya kila aina vitakuwa kwa ajili ya makuhani. Tena mutawapa sehemu ya kwanza ya unga wenu, kusudi mulete baraka juu ya nyumba zenu.