Ezekiel 44:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Hakuna mtu yeyote wa taifa geni, asiyetahiriwa au asiyenitii mimi, atakayeruhusiwa kuingia maskani yangu; hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli, hawataruhusiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Hakuna mtu yeyote wa taifa geni, asiyetahiriwa au asiyenitii mimi, atakayeruhusiwa kuingia maskani yangu; hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli, hawataruhusiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana Mwenyezi asemalo: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Hakuna mtu yeyote wa taifa geni, asiyetahiriwa au asiyenitii mimi, atakayeruhusiwa kuingia maskani yangu; hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli, hawataruhusiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Mgeni yeyote asiyetahiriwa wala moyo wala mwili asipaingie tena Patakatifu pangu, ijapo awe mmoja wao wale wageni wote wakaao kwa wana wa Isiraeli katikati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, Bwana wetu Yawe anasema hivi: Hakuna mutu yeyote wa taifa la kigeni, asiyetahiriwa au asiyenitii mimi atakayeruhusiwa kuingia katika hekalu langu; hata wageni wanaoishi kati ya Waisraeli, hawataruhusiwa.