Ezekiel 45:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtakapoigawanya nchi kwa kura ili kila kabila lipate sehemu yake, sehemu moja ya nchi ni lazima iwekwe wakfu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu. Urefu wake utakuwa kilomita kumi na mbili u nusu na upana wa kilomita kumi. Eneo hilo lote litakuwa takatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa Mwenyezi Mungu kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wake dhiraa elfu ishirini; eneo hili lote litakuwa takatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea Bwana toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi ishirini na tano elfu, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtakapoigawanya nchi kwa kura ili kila kabila lipate sehemu yake, sehemu moja ya nchi ni lazima iwekwe wakfu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu. Urefu wake utakuwa kilomita kumi na mbili u nusu na upana wa kilomita kumi. Eneo hilo lote litakuwa takatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa BWANA kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa 25,000 upana wake dhiraa 20,000, eneo hili lote litakuwa takatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa bwana kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa 25,000, upana wake dhiraa 20,000 eneo hili lote litakuwa takatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea BWANA toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi elfu ishirini na tano, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtakapoigawanya nchi kwa kura ili kila kabila lipate sehemu yake, sehemu moja ya nchi ni lazima iwekwe wakfu kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu. Urefu wake utakuwa kilomita kumi na mbili u nusu na upana wa kilomita kumi. Eneo hilo lote litakuwa takatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakapopiga kura za kujigawanyia mafungu ya nchi hii, mtatoa kwanza katika nchi hii kipande cha kumpa Bwana kuwa Patakatifu, urefu wake uwe mianzi 25000, nao upana wake uwe mianzi 10000; hapo sharti pawe Patakatifu katika mipaka yake yote ipazungukayo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, mtakapoigawanya nchi kwa kura iwe urithi, mtamtolea BWANA toleo, sehemu takatifu ya nchi, urefu wake utakuwa urefu wa mianzi ishirini na tano elfu, na upana wake elfu kumi; itakuwa takatifu ndani ya mipaka yake yote pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutakapoigawanya inchi kwa kupiga kura kusudi kila kabila lipate sehemu yake, sehemu moja ya inchi ni lazima itakaswe kwa ajili ya Yawe. Urefu wake utakuwa kilometre kumi na mbili na nusu na upana kilometre kumi. Eneo hilo lote litakuwa takatifu.