Ezekiel 45:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kipimo cha ulinganifu: Efa kwa nafaka na bathi kwa mafuta zina kiasi sawa. Hivyo viwili ni moja ya kumi ya homeri moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Efa na bathi viwe sawa, bathi iwe sehemu ya kumi ya homeri na efa iwe sehemu ya kumi ya homeri, homeri itakuwa ndicho kiwango cha kukubalika kwa vyote viwili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Efa na bathi zitakuwa za kipimo kimoja; ili kwamba bathi ichukue sehemu ya kumi ya homeri, na efa sehemu ya kumi ya homeri; kipimo chake kitakuwa kwa kadiri ya cheo cha kawaida cha homeri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kipimo cha ulinganifu: efa kwa nafaka na bathi kwa mafuta zina kiasi sawa. Hivyo viwili ni moja ya kumi ya homeri moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Efa na bathi viwe sawa, bathi iwe sehemu ya kumi ya homeri na efa iwe sehemu ya kumi ya homeri, homeri itakuwa ndicho kiwango cha kukubalika kwa vyote viwili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Efa na bathi viwe sawa, bathi iwe sehemu ya kumi ya homeri na efa iwe sehemu ya kumi ya homeri, homeri itakuwa ndicho kiwango cha kukubalika kwa vyote viwili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Efa na bathi zitakuwa za kipimo kimoja; ili kwamba bathi ichukue sehemu ya kumi ya homeri, na efa sehemu ya kumi ya homeri; kipimo chake kitakuwa kwa kadiri ya cheo cha kawaida cha homeri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kipimo cha ulinganifu: Efa kwa nafaka na bathi kwa mafuta zina kiasi sawa. Hivyo viwili ni moja ya kumi ya homeri moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pishi moja na vibaba vinne sharti viwe kipimo kimoja sawasawa, vibaba vinne vipate kuwa fungu la sita la frasila, vilevile pishi moja iwe fungu la sita la frasila; hivyo frasila itatumika ya kulinganisha vipimo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Efa na bathi zitakuwa za kipimo kimoja; ili kwamba bathi ichukue sehemu ya kumi ya homeri, na efa sehemu ya kumi ya homeri; kipimo chake kitakuwa kwa kadiri ya cheo cha kawaida cha homeri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa kipimo cha ulinganifu: efa kwa unga na bati kwa mafuta zina kipimo sawasawa. Hivyo viwili ni sehemu moja ya kumi ya homeri moja.