Ezekiel 45:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika eneo hilo utapima pia sehemu yenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kwa kilomita tano; humo kutakuwa maskani yangu, mahali patakatifu kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa elfu ishirini na tano, na upana wa dhiraa elfu kumi. Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, ndipo Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa kipimo hicho utapima, urefu wa ishirini na tano elfu, na upana wa elfu kumi; na ndani yake patakuwa patakatifu, palipo patakatifu sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika eneo hilo utapima pia sehemu yenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kwa kilomita tano; humo kutakuwa maskani yangu, mahali patakatifu kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa kipimo hicho utapima, urefu wa elfu ishirini na tano, na upana wa elfu kumi; na ndani yake patakuwa patakatifu, palipo patakatifu sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika eneo hilo utapima pia sehemu yenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kwa kilomita tano; humo kutakuwa maskani yangu, mahali patakatifu kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mahali hapo palipopimwa utapapima tena urefu wa mianzi 25000 na upana wa mianzi 10000, napo hapo ndipo pajengwe Patakatifu patakapokuwa Patakatifu Penyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa kipimo hicho utapima, urefu wa ishirini na tano elfu, na upana wa elfu kumi; na ndani yake patakuwa patakatifu, palipo patakatifu sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika eneo hilo utapima vilevile sehemu yenye urefu wa kilometre kumi na mbili na nusu kwa kilometre tano; humo kutakuwa hekalu langu, Pahali Patakatifu Sana.