Ezekiel 45:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Eneo hilo litakuwa takatifu nchini, na kutengwa kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Mwenyezi-Mungu katika maskani yake. Ndani ya eneo hilo kutakuwa na nyumba zao na nafasi iliyowekwa wakfu kwa ajili ya maskani yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za Mwenyezi Mungu. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hiyo ni sehemu takatifu ya nchi; itakuwa ya makuhani, wahudumu wa patakatifu, wakaribiao kumhudumia Bwana; nayo itakuwa mahali kwa nyumba zao, na patakatifu kwa mahali patakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Eneo hilo litakuwa takatifu nchini, na kutengwa kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Mwenyezi-Mungu katika maskani yake. Ndani ya eneo hilo kutakuwa na nyumba zao na nafasi iliyowekwa wakfu kwa ajili ya maskani yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za BWANA. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za bwana. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hiyo ni sehemu takatifu ya nchi; itakuwa ya makuhani, wahudumu wa patakatifu, wakaribiao kumhudumia BWANA; nayo itakuwa mahali kwa nyumba zao, na patakatifu kwa mahali patakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Eneo hilo litakuwa takatifu nchini, na kutengwa kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Mwenyezi-Mungu katika maskani yake. Ndani ya eneo hilo kutakuwa na nyumba zao na nafasi iliyowekwa wakfu kwa ajili ya maskani yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nchi hiyo itakuwa takatifu, iwe yao watambikaji wanaofanya kazi za utumishi wa Patakatifu wakimkaribia Bwana na kumtumikia; kwa hiyo mahali hapo patakuwa pao pa nyumba zao, napo patakuwa patakatifu penye hapo Patakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hiyo ni sehemu takatifu ya nchi; itakuwa ya makuhani, wahudumu wa patakatifu, wakaribiao kumhudumia BWANA; nayo itakuwa mahali kwa nyumba zao, na patakatifu kwa mahali patakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Eneo hilo litakuwa takatifu katika inchi, na kutengwa kwa ajili ya makuhani wanaomutumikia Yawe katika hekalu lake. Ndani ya eneo hilo kutakuwa nyumba zao na nafasi iliyotakaswa kwa ajili ya hekalu langu.