Ezekiel 45:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtawala, naye atapewa eneo lake upande wa mashariki na magharibi wa eneo lililowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Eneo hilo litaenea magharibi mpaka bahari ya Mediteranea na upande wa mashariki hadi mpaka wa mashariki wa nchi. Litakuwa na urefu sawa na eneo lililopewa kila kabila la Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Mkuu anayetawala atakuwa na eneo linalopakana na lile eneo lililowekwa wakfu kwa upande moja, na eneo la mji upande mwingine. Eneo la mji litaenea upande wa magharibi kuanzia upande wa magharibi, na kuenea mashariki kuanzia upande wa mashariki, likiendelea kwa urefu kutoka magharibi hadi mpaka wa mashariki, sambamba na mojawapo ya sehemu za makabila.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sehemu itakayokuwa ya mkuu itakuwa upande huu, na upande huu, wa toleo takatifu, na wa milki ya mji, kulikabili toleo takatifu, na kuikabili milki ya mji, upande wa magharibi kuelekea magharibi, na upande wa mashariki kuelekea mashariki; na kwa urefu wake sawasawa na sehemu mojawapo, toka mpaka wa magharibi hata mpaka wa mashariki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtawala, naye atapewa eneo lake upande wa mashariki na magharibi wa eneo lililowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Eneo hilo litaenea magharibi mpaka bahari ya Mediteranea na upande wa mashariki hadi mpaka wa mashariki wa nchi. Litakuwa na urefu sawa na eneo lililopewa kila kabila la Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Mkuu anayetawala atakuwa na lile eneo linalopakana na lile eneo lililowekwa wakfu upande huu na upande huu na eneo la mji. Eneo la mji litaenea upande wa magharibi kuanzia upande wa magharibi na upande wa mashariki kuanzia upande wa mashariki, likiendelea kwa urefu kutoka magharibi hadi mpaka wa mashariki sambamba na mojawapo ya sehemu za makabila.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Mkuu anayetawala atakuwa na lile eneo linalopakana na lile eneo lililowekwa wakfu upande huu na upande huu na eneo la mji. Eneo la mji litaenea upande wa magharibi kuanzia upande wa magharibi na upande wa mashariki kuanzia upande wa mashariki, likiendelea kwa urefu kutoka magharibi hadi mpaka wa mashariki sambamba na mojawapo ya sehemu za makabila.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sehemu itakayokuwa ya mkuu itakuwa upande huu, na upande huu, wa toleo takatifu, na wa milki ya mji, kulikabili toleo takatifu, na kuikabili milki ya mji, upande wa magharibi kuelekea magharibi, na upande wa mashariki kuelekea mashariki; na kwa urefu wake sawasawa na sehemu mojawapo, toka mpaka wa magharibi hadi mpaka wa mashariki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtawala, naye atapewa eneo lake upande wa mashariki na magharibi wa eneo lililowekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Eneo hilo litaenea magharibi mpaka bahari ya Mediteranea na upande wa mashariki hadi mpaka wa mashariki wa nchi. Litakuwa na urefu sawa na eneo lililopewa kila kabila la Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mkuu mtampa huku na huko penye kile kipande kitakatifu napo penye pake mji mbele ya kipande kitakatifu na mbele ya hapo palipo pake mji paelekeapo baharini upande wa kwenda baharini napo paelekeapo maawioni kwa jua, urefu wake ulingane na urefu wa fungu moja wa mafungu ya mashina toka mpaka wa baharini hata mpaka wa nchi uelekeao maawioni kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sehemu itakayokuwa ya mkuu itakuwa upande huu, na upande huu, wa toleo takatifu, na wa milki ya mji, kulikabili toleo takatifu, na kuikabili milki ya mji, upande wa magharibi kuelekea magharibi, na upande wa mashariki kuelekea mashariki; na kwa urefu wake sawasawa na sehemu mojawapo, toka mpaka wa magharibi hata mpaka wa mashariki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukubwa, naye atapewa eneo lake upande wa mashariki na magaribi wa eneo lililotakaswa kwa ajili ya Yawe. Eneo hilo litaenea tangia upande wa magaribi mpaka kwenye bahari ya Mediteranea na upande wa mashariki mpaka upande wa mashariki wa inchi. Litakuwa na urefu sawa na eneo lililopewa kwa kila kabila la Waisraeli.