Ezekiel 45:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hiyo ndiyo milki ya mtawala katika Israeli. Hivyo mtawala hatawadhulumu watu wangu, bali ataacha nchi igawiwe Waisraeli kulingana na makabila ya Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nchi hii itakuwa milki yake katika Israeli. Nao wakuu wangu hawatawadhulumu tena watu wangu, bali watairuhusu nyumba ya Israeli kuimiliki nchi kulingana na makabila yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika nchi hiyo itakuwa milki kwake katika Israeli; wala wakuu wangu hawatawaonea watu wangu tena kabisa; bali watawapa nyumba ya Israeli nchi hiyo, kwa kadiri ya makabila yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hiyo ndiyo milki ya mtawala katika Israeli. Hivyo mtawala hatawadhulumu watu wangu, bali ataacha nchi igawiwe Waisraeli kulingana na makabila ya Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nchi hii itakuwa milki yake katika Israeli. Nao wakuu wangu hawataonea tena watu wangu bali watairuhusu nyumba ya Israeli kuimiliki nchi kulingana na makabila yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nchi hii itakuwa milki yake katika Israeli. Nao wakuu wangu hawataonea tena watu wangu bali watairuhusu nyumba ya Israeli kuimiliki nchi kulingana na makabila yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika nchi hiyo itakuwa milki kwake katika Israeli; wala wakuu wangu hawatawaonea watu wangu tena kabisa; bali watawapa nyumba ya Israeli nchi hiyo, kwa kadiri ya makabila yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hiyo ndiyo milki ya mtawala katika Israeli. Hivyo mtawala hatawadhulumu watu wangu, bali ataacha nchi igawiwe Waisraeli kulingana na makabila ya Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo patakuwa mali zake za kupashika kuwa pake kwa Waisiraeli, wakuu wangu wasiwakorofishe tena walio ukoo wangu, nayo nchi watawapa walio mlango wa Isiraeli ya kuyagawia mashina yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika nchi hiyo itakuwa milki kwake katika Israeli; wala wakuu wangu hawatawaonea watu wangu tena kabisa; bali watawapa nyumba ya Israeli nchi hiyo, kwa kadiri ya makabila yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huo ndio urizi wa mufalme katika Israeli. Hivyo mufalme hatawatesa watu wangu, lakini ataacha inchi igawanywe kwa Waisraeli kulingana na makabila ya Israeli.